0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

650. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwa Na Ghadhabu Yanapokeukwa Matakatifu Ya Allah Na Kuinusuru Dini Yake

باب الغضب إِذَا انتهكت حرمات الشّرع والانتصار لدين الله تعالى


وعن عائشة رضي الله عنها: أن قرَيشاً أهَمَّهُمْ شَأنُ المَرأَةِ المخزومِيَّةِ الَّتي سَرَقَتْ، فقالوا: مَنْ يُكَلِّمُ فِيهَا رسول الله – صلى الله عليه وسلم -؟ فقالوا: مَنْ يَجْتَرِئ عَلَيْهِ إِلاَّ أُسَامَةُ بنُ زَيْدٍ حِبُّ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -؟ فَكَلَّمَهُ أُسَامَةُ، فَقَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: { أتَشْفَعُ في حَدٍّ مِنْ حُدُودِ الله تَعَالَى؟!} ثُمَّ قامَ فَاخْتَطَبَ، ثُمَّ قَالَ: { إنَّمَا أهْلَك مَنْ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ، وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ أقامُوا عَلَيْهِ الحَدَّ، وَايْمُ الله، لَوْ أَنَّ فَاطمَةَ بِنْتَ مُحمّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعتُ يَدَهَا}     متفقٌ عَلَيْهِ.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Maqureshi walipatwa na hamu kuhusiana na habari ya mwanamke wa kabila la Makhzum aliyeiba. Wakauliza: “Ni nani atakayemzungumzia Mtume (ﷺ) jambo hili?” Wakasema: “Hapana mwenye ujasiri ela ni Usâma bin Zaid, kipenzi cha Mtume (ﷺ)  ” Usâma akasema naye. Mtume (ﷺ) akamwambia: “Unashufaiya (unaombea) katika haddi (adhabu) miongoni mwa haddi za Allâh?” Halafu akasimama kuwakhutubia watu: “Kwa yakini, waliangamia waliokuwa kabla yenu. Kwamba wao, anapoiba mwenye sharafu (utukufu) katika wao, wanamuacha. Na mtu dhaifu akiiba, wanamsimamishia haddi. Naapa kwa Allâh! Lau Fâtima binti Muhammad angaliiba, ningaliukata mkono wake!”     [ Wameafikiana Bukhari na Muslim].   


Begin typing your search above and press return to search.