0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

65. MLANGO WA KUKUMBUKA MAUTI NA KUPUNGUZA TAMAA

باب ذكر الموت وقصر الأمل


قَالَ الله تَعَالَى: ﴿كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَمَا الحَياةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُورِ﴾ [ آل عمران: 185 ]

وقال تَعَالَى: ﴿وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَاذَا تَكْسِبُ غَدَاً وَمَا تَدْري نَفْسٌ بأيِّ أرْضٍ تَمُوتُ﴾ [ لقمان: 34 ]

وقال تَعَالَى: ﴿فَإذَا جَاءَ أجَلُهُمْ لاَ يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلاَ يَسْتَقْدِمُونَ﴾ [ النحل: 61 ]]

وقال تَعَالَى: ﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تُلْهِكُمْ أمْوَالُكُمْ وَلاَ أوْلاَدُكُمْ عَنْ ذِكْرِ الله وَمَنْ يَفْعَلْ ذَلِكَ فَأُولئِكَ هم الْخَاسِرُونَ وَأنْفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُمْ مِنْ قَبْلِ أنْ يَأتِيَ أَحَدَكُمُ المَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلاَ أخَّرْتَنِي إِلَى أَجَلٍ قَريبٍ فَأصَّدَّقَ وأَكُنْ مِنَ الصَّالِحِينَ وَلَنْ يُؤَخِّرَ اللهُ نَفْساً إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا وَاللهُ خَبيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴾ [ المنافقون: 9-11 ]

وقال تَعَالَى: ﴿حَتَّى إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ المَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ لَعَلّي أعْمَلُ صَالِحاً فِيمَا تَرَكْتُ كَلاَّ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا وَمِنْ وَرَائِهِمْ بَرْزَخٌ إِلَى يَوْمِ يبْعَثُونَ فَإذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلاَ أنْسَابَ بَيْنَهُمْ يَومَئِذٍ وَلاَ يَتَسَاءلُونَ فَمَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأولئِكَ الَّذِينَ خَسرُوا أَنْفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ تَلْفَحُ وَجَوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَى عَلَيْكُمْ فَكُنْتُمْ بِهَا تُكَذِّبُونَ﴾ إِلَى قَوْله تَعَالَى: ﴿… كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ قَالُوا لَبِثْنَا يَوْماً أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْئَلِ العَادِّينَ قَالَ إنْ لَبِثْتُمْ إِلاَّ قَلِيلاً لَوْ أَنَّكُمْ كُنْتُم تَعْلَمُونَ أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثاً وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لاَ تُرْجَعُونَ﴾ [ المؤمنون: 99-115 ]

وقال تَعَالَى: ﴿أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلاَ يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِم الأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ﴾ [ الحديد: 16 ]

وَالآيات في الباب كَثيرةٌ معلومة


شرح الحديث على آيات الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى





65. MLANGO WA KUKUMBUKA MAUTI NA KUPUNGUZA TAMAA


Mwenyezi Mungu Amesema: “Kila nafsi itaonja mauti. Na bila shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyama. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.”   [3:185].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani.”   [31:34].

Mwenyezi Mungu Amesema:  “Na unapofika muda wao hawatakawilia hata saa moja wala hawatatangulia.”   [16:34].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Enyi mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Allâh; na wafanyao hayo, hao ndio wenye kukhasirika. Na toeni katika yale Tuliyowapa kabla mmoja wenu hayajamjia mauti, kisha akasema: “Mola wangu! Huniakhirishi muda kidogo (tu) nikatoa sadaka na nikawa miongoni mwa watendao mema?” Lakini Allâh Hataiakhirisha nafsi yoyote inapokuja ajali yake; na Allâh Anazo habari za mnayoyatenda (yote).”   [63:9-11].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe. Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapofufuliwa. Basi litakapopulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana. Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu. Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizokunjana. Je! Hazikuwa Aya Zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?” Mpaka Aliposema: “Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingelikuwa mnajua. Je! Mlidhani ya kwamba Tuliwaumba bure na ya kwamba nyinyi Kwetu hamtarudishwa?”   [23:99-115].

Mwenyezi Mungu Amesema: “Je! Wakati haujafika tu wale walioamini kwamba nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Allâh na kwa mambo ya haki yaliyoteremka? Wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu zamani (Mayahudi na Manasara), na muda wao (wa kuondokewa na Mitume) ukawa mrefu; kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa waasi.”   [57:16].

Aya zinazoeleza mambo haya ni nyingi, mashuhuri.


Begin typing your search above and press return to search.