باب استحباب العزلة عند فساد الناس والزمان أَو الخوف من فتنة في الدين ووقوع في حرام وشبهات ونحوها
وعن أَبي سعيد الخدري – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رَجُلٌ: أيُّ النَّاسِ أفْضَلُ يَا رسولَ الله؟ قَالَ: { مُؤْمِنٌ مُجَاهِدٌ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ في سَبيلِ اللهِ} قَالَ: ثُمَّ مَنْ؟ قَالَ: { ثُمَّ رَجُلٌ مُعْتَزِلٌ فِي شِعْبٍ مِنَ الشِّعَابِ يَعْبُدُ رَبَّهُ}
وفي رواية: { يَتَّقِي اللهَ، وَيَدَعُ النَّاسَ مِنْ شَرِّهِ} متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Sa‘îd al-Khudry (Radhi za Allah ziwe juu yake) amehadithia: “Mtu mmoja aliuliza: “Yâ Rasûlallâh, mtu yupi ni bora?” Akamjibu: “Mwumini mpiganaji Jihadi kwa nafsi yake na mali yake katika Njia ya Allâh.” Akauliza: “Kisha ni yupi?” Akamjibu: “Kisha ni mtu aliejitenga katika bonde miongoni mwa mabonde akimwabudu Mola wake.”
Riwaya nyingine imesema: “..anamcha Allâh na anawaepushia watu shari yake.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]