باب الورع وترك الشبهات
وعن النعمان بن بشيرٍ – رضي الله عنهما -، قَالَ: سَمِعْتُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: { إنَّ الحَلاَلَ بَيِّنٌ، وَإنَّ الحَرامَ بَيِّنٌ، وَبَيْنَهُمَا مُشْتَبَهَاتٌ لاَ يَعْلَمُهُنَّ كَثيرٌ مِنَ النَّاسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ، اسْتَبْرَأَ لِدِينهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ فِي الشُّبُهَاتِ وَقَعَ في الحَرَامِ، كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الحِمَى يُوشِكُ أنْ يَرْتَعَ فِيهِ، ألاَ وَإنَّ لكُلّ مَلِكٍ حِمَىً، ألاَ وَإنَّ حِمَى اللهِ مَحَارِمُهُ، ألاَ وَإنَّ فِي الجَسَدِ مُضْغَةً إِذَا صَلَحَت صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، وَإِذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، ألاَ وَهِيَ القَلْبُ} متفقٌ عَلَيْهِ، وروياه مِنْ طرقٍ بِألفَاظٍ متقاربةٍ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
68. MLANGO WA UCHAMUNGU NA KUACHA SHUBHA (YENYE KUTIA SHAKA)
Imepokewa kutoka kwa An-Nu’mân bin Bashîr (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Hakika, halali iko dhahiri na haramu iko dhahiri. Baina ya mawili hayo, muna yenye kutia shaka. Wengi katika watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. Na atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haramu. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo (kwingine). Fahamuni! kila mfalme ana mipaka. Fahamuni! Kwa yakini mipaka ya Allâh ni haramu Alizoharamisha. Fahamuni! Kwa yakini katika mwili muna kinofu (cha nyama), kinapokuwa sahihi, mwili wote unakuwa sahihi. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Fahamuni! Kinofu hicho ni: moyo.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ]