0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

579. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kukumbuka Mauti Na Kupunguza Tamaa.

باب ذكر الموت وقصر الأمل


وعن أُبَيِّ بن كعبٍ – رضي الله عنه -: كَانَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – إِذَا ذَهَبَ ثُلُثُ اللَّيْلِ قَامَ، فَقَالَ: { يَا أَيُّهَا النَّاسُ، اذْكُرُوا اللهَ، جَاءتِ الرَّاجِفَةُ، تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ، جَاءَ المَوْتُ بِمَا فِيهِ، جَاءَ المَوْتُ بِمَا فِيهِ} قُلْتُ: يَا رسول الله، إنِّي أُكْثِرُ الصَّلاَةَ عَلَيْكَ، فَكَمْ أجْعَلُ لَكَ مِنْ صَلاَتِي؟ فَقَالَ: { مَا شِئْتَ} قُلْتُ: الرُّبُع، قَالَ: { مَا شِئْتَ، فَإنْ زِدْتَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ} قُلْتُ: فَالنِّصْف؟ قَالَ: { مَا شِئْتَ، فَإنْ زِدْتَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ} قُلْتُ: فالثُّلُثَيْنِ؟ قَالَ: { مَا شِئْتَ، فَإنْ زِدْتَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ} قُلْتُ: أجعَلُ لَكَ صَلاَتِي كُلَّهَا؟ قَالَ: { إذاً تُكْفى هَمَّكَ، وَيُغْفَر لَكَ ذَنْبكَ}   رواه الترمذي، وقال: {حديث حسن}.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Ubayyi bin Ka’b  (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume  alikuwa unapopita thuluthi ya usiku huamka na akisema: “Enyi watu! Mtajeni Allâh. Limefika baragumu la kwanza linalofwatiwa na baragumu la pili. Mauti yamekuja na misiba yake, mauti yamekuja na misiba yake.” Nikamwambia: “Yâ Rasûlallâh, mimi huzidisha kukuswalia, nikuswalie mara ngapi katika dua zangu?” Akanambia: “Unavyopenda.” Nikamwuliza: “Robo (ya dua zangu)?” Akajibu: “Upendavyo, ukizidisha ni kheri kwako.” Nikamwambia: “Nusu.” Akasema: “Upendavyo, ukizidisha ni kheri kwako.” Nikamwambia: “Thuluthi mbili.” Akasema: “Upendavyo, ukizidisha ni kheri kwako.” Nikamwambia: “Dua yangu yote nitaifanya iwe ni kukuswalia.” Akanambia: “Ukifanya hivyo, utatoshelezewa hamu yako na utasamehewa dhambi zako.”    [ Imepokewa naTirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]

Begin typing your search above and press return to search.