0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

561. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Ukarimu Ufadhili Na Kutoa Katika Njia Za Kheri Kwa Kumwamini Allah Mtukufu.

باب الكرم والجود والإنفاق في وجوه الخير ثقةً بالله تعالى


وعن أَبي هريرة – رضي الله وعنه، عن النبيِّ – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: { بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِفَلاَةٍ مِنَ الأَرْضِ، فَسَمِعَ صَوْتاً في سَحَابَةٍ، اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ، فَتَنَحَّى ذَلِكَ السَّحَابُ فَأفْرَغَ مَاءهُ في حَرَّةٍ، فإِذَا شَرْجَةٌ مِنْ تِلْكَ الشِّرَاجِ قَدِ اسْتَوْعَبَت ذَلِكَ الماءَ كُلَّهُ، فَتَتَبَّعَ المَاءَ، فإذَا رَجُلٌ قَائمٌ في حَدِيقَتِهِ يُحَوِّلُ الماءَ بِمسحَاتِهِ، فَقَالَ لَهُ: يَا عَبْدَ اللهِ، ما اسمُكَ؟ قال: فُلانٌ للاسم الذي سَمِعَ في السَّحابةِ، فقال له: يا عبدَ الله، لِمَ تَسْألُنِي عَنِ اسْمِي؟ فَقَالَ: إنِّي سَمِعْتُ صَوتْاً في السَّحابِ الَّذِي هَذَا مَاؤُهُ، يقولُ: اسْقِ حَدِيقَةَ فُلاَنٍ لاسمِكَ، فَمَا تَصْنَعُ فِيهَا، فَقَالَ: أمَا إذ قلتَ هَذَا، فَإنِّي أنْظُرُ إِلَى مَا يَخْرُجُ مِنْهَا، فَأتَصَدَّقُ بِثُلُثِهِ، وَآكُلُ أنَا وَعِيَالِي ثُلُثاً، وَأردُّ فِيهَا ثُلُثَهُ}     رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ amesimulia: “Alikuwepo mtu mmoja anatembea katika jangwa, mara akasikia sauti katika wingu ikisema: “Nyosheleza bustani la fulani.” Wingu lile likasogea na likamimina maji kwenye ardhi yenye mawe meusi, halafu kukawa kuna korongo (mahala palipo na mfereji mkubwa utokanao na mvua kubwa au mto) ambapo maji yote hujikusanya hapo. Akayafwatilia maji yale, mara akamuona mtu amesimama katika bustani yake akiyaelekeza maji kwa beleshi (chombo kitumikacho kuchotea mchanga, udongo na kadhalika) lake. Akamwuliza: “Ee mja wa Allâh, nani jina lako?” Akamjibu: “Naitwa fulani,” akamtajia jina alilolisikia katika wingu lile. Naye akamwuliza: “Ee mja wa Allâh, kwa nini umeniuliza jina langu?” Akamjibu: “Mimi nilisikia sauti katika wingu ambalo haya ndio maji yake ikisema “nyosheleza katika bustani la fulani,” ikitaja jina lako, kwani huwa wafanya nini katika bustani yako?” Akamwambia: “Ama kwa kuwa umesema hivyo, basi mimi (nitakueleza ninalotenda), hutazama kinachotoka humo, nikatoa sadaka thuluthi yake, mimi na familia yangu tukala thuluthi moja, na thuluthi nyingine huirudisha humo (kuligharamikia).”    [ Imepokewa na Muslim.]

Begin typing your search above and press return to search.