باب الكرم والجود والإنفاق في وجوه الخير ثقةً بالله تعالى
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -: أنَّه سمع رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، يَقولُ: { مَثَل البَخيل وَالمُنْفِقِ، كَمَثَلِ رَجُلَيْنِ عَلَيْهِمَا جُنَّتَانِ مِنْ حَديد مِنْ ثُدِيِّهِمَا إِلَى تَرَاقِيهِمَا، فَأَمَّا المُنْفِقُ فَلاَ يُنْفِقُ إِلاَّ سَبَغَتْ – أَوْ وَفَرَتْ – عَلَى جِلْدِهِ حَتَّى تُخْفِيَ بَنَانَهُ، وَتَعْفُو أثرَهُ، وأمَّا البَخِيلُ، فَلاَ يُريدُ أنْ يُنْفِقَ شَيْئاً إِلاَّ لَزِقَتْ كُلُّ حَلْقَةٍ مَكَانَهَا، فَهُوَ يُوسِّعُهَا فَلاَ تَتَّسِعُ} متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amemsikia Mtume ﷺ akisema: “Mfano wa mtu bakhili na mtoaji ni mfano wa watu wawili waliovaa deraya ya chuma kuanzia vifuani mpaka katika mitulinga (mfupa wa mbele wa bega) yao. Ama yule atoaye anapotoa deraya yake hufunguliwa na huwa ndefu juu yake hata huvificha vidole vyake na miguu yake na hufuta alama ya miguu yake. Ama bakhili anapoazimia kutoa kila duara ya deraya yake huzama mahali pake. Yeye hujaribu kuipanua lakini haipanuki.” [ Imepokewa na Bukhârî.]