باب الكرم والجود والإنفاق في وجوه الخير ثقةً بالله تعالى
وعن أَبي كبشة عمرو بن سعد الأنماري – رضي الله عنه -: أنّه سمع رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: { ثَلاَثَةٌ أُقْسمُ عَلَيْهِنَّ، وَأُحَدِّثُكُمْ حَدِيثاً فَاحْفَظُوهُ: مَا نَقَصَ مَالُ عَبْدٍ مِنْ صَدَقَةٍ، وَلاَ ظُلِمَ عَبْدٌ مَظْلَمَةً صَبَرَ عَلَيْهَا إِلاَّ زَادَهُ اللهُ عِزّاً، وَلاَ فَتَحَ عَبْدٌ بَابَ مَسألَةٍ إِلاَّ فَتَحَ اللهُ عَلَيْهِ بَابَ فَقرٍ – أَوْ كَلِمَةً نَحْوَهَا – وَأُحَدِّثُكُمْ حَديثاً فَاحْفَظُوهُ، قَالَ: { إنَّمَا الدُّنْيَا لأرْبَعَةِ نَفَرٍ: عَبْدٍ رَزَقَهُ اللهُ مَالاً وَعِلماً، فَهُوَ يَتَّقِي فِيهِ رَبَّهُ، وَيَصِلُ فِيهِ رَحِمَهُ، وَيَعْلَمُ للهِ فِيهِ حَقَّاً، فَهذا بأفضَلِ المَنَازِلِ. وَعَبْدٍ رَزَقهُ اللهُ عِلْماً، وَلَمْ يَرْزُقْهُ مَالاً، فَهُوَ صَادِقُ النِّيَّةِ، يَقُولُ: لَوْ أنَّ لِي مَالاً لَعَمِلتُ بِعَمَلِ فُلانٍ، فَهُوَ بنيَّتِهِ، فأجْرُهُمَا سَوَاءٌ. وَعَبْدٍ رَزَقَهُ الله مَالاً، وَلَمَ يَرْزُقْهُ عِلْماً، فَهُوَ يَخبطُ في مَالِهِ بغَيرِ عِلْمٍ، لاَ يَتَّقِي فِيهِ رَبَّهُ، وَلاَ يَصِلُ فِيهِ رَحِمَهُ، وَلاَ يَعْلَمُ للهِ فِيهِ حَقّاً، فَهذَا بأَخْبَثِ المَنَازِلِ. وَعَبْدٍ لَمْ يَرْزُقْهُ اللهُ مَالاً وَلاَ عِلْماً، فَهُوَ يَقُولُ: لَوْ أنَّ لِي مَالاً لَعَمِلْتُ فِيهِ بعَمَلِ فُلاَنٍ، فَهُوَ بنِيَّتِهِ، فَوِزْرُهُمَا سَوَاءٌ} رواه الترمذي، وقال: {حديث حسن صحيح}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Kabshah, ‘Amri bin Sa’d al-Anmâry (Radhi za Allah ziwe juu yake) alimsikia Mtume ﷺ akisema: “Mambo matatu nayaapia, na nitawazungumzia mazungumzo yahifadhini: Mali ya mtu hayapungui kwa kutoa sadaka, yeyote atakayedhulumiwa na akasubiri, Allâh Humzidishia utukufu, na wala mtu hatafungua mlango wa kuomba ispokuwa Allâh Atamfungulia mlango wa ufukara,” au alisema neno kama hilo. “Nawahadithia mazungumzo yahifadhini: Hakika dunia ni ya watu wanne: (1) Mja ambaye, Allâh Amemruzuku mali na ilimu, akawa anamcha Mola wake katika mali hiyo, anaunga kizazi chake (akiwasaidia jamaa zake) na anaijua haki ya Allâh katika mali hiyo. Mtu huyu yuko katika daraja bora kabisa. (2) Mja ambaye, Allâh Amemruzuku ilimu wala Hakumruzuku mali, akawa ana niya ya kweli, anasema: “Lau ningalikuwa nina mali, ningalifanya kama fulani,” yeye atalipwa kwa niya yake, na ujira wao ni sawa kwa sawa. (3) Mja ambaye, Allâh Amemruzuku mali wala Hakumruzuku ilimu, akawa anayachezea mali yake bila ya ujuzi, hamchi Mola wake katika mali hiyo, haungi kizazi chake kwa mali hiyo wala haijui haki ya Allâh katika mali hiyo, mtu huyu yuko katika daraja mbaya zaidi. (4) Mja ambaye, Allâh Hakumruzuku mali wala ilimu, anasema: “Lau ningalikuwa nina mali ningalifanya kama fulani (anayetenda mabaya),” basi yeye atalipwa kwa niya yake, na dhambi zao ni sawa kwa sawa.” [ Imepokewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan Sahîh.]