باب الجمع بين الخوف والرجاء
قَالَ الله تَعَالَى: ﴿فَلاَ يَأمَنُ مَكْرَ الله إِلاَّ القَوْمُ الخَاسِرونَ﴾ [ الأعراف: 99 ]
وقال تَعَالَى: ﴿إِنَّهُ لاَ يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللهِ إِلاَّ القَوْمُ الكافِرُونَ﴾ [ يوسف: 87 ]
وقال تَعَالَى: ﴿يَوْمَ تَبْيَضُّ وَجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ﴾ [ آل عمران: 106 ]
وقال تَعَالَى: ﴿إنَّ رَبَكَ لَسَرِيعُ العِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَحِيمٌ﴾ [ الأعراف: 166 ]
وقال تَعَالَى: ﴿إنَّ الأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ وَإِنَّ الفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ﴾ [ الانفطار: 13-14 ]
وقال تَعَالَى: ﴿فَأمَّا مَنْ ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ وَأمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأمُّهُ هَاوِيَةٌ﴾ [ القارعة: 6-9 ] والآيات في هذا المعنى كثيرةٌ. فَيَجْتَمعُ الخَوفُ والرجاءُ في آيَتَيْنِ مُقْتَرِنَتَيْنِ أَو آيات أَو آية
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
53. MLANGO WA KUJUMUISHA BAINA YA KHOFU NA MATARAJIO
Mwenyezi Mungu Amesema: [ Je, wameaminisha kuadhibiwa na Allâh? Hawaaminishi adhabu ya Allâh ila watu ambao (watakuwa) wenye hasara.] [7:99].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ Hakika hawakati tamaa na faraji ya Allâh isipokuwa watu makafiri.] [12:87].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ Siku ambayo nyuso zitakuwa nyeupe, na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. [3:106].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu.] [7:167].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ Kwa hakika wafanyao wema watakuwa neemani. Na waovu watakuwa motoni. ] [82:13, 14].
Mwenyezi Mungu Amesema: [ Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, huyo atakuwa katika maisha yanayompendeza. Na yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, huyo maskani yake yatakuwa katika (huo moto) Hâwiyah.] [101:6-9].