باب القناعة والعَفاف والاقتصاد في المعيشة والإنفاق وذم السؤال من غير ضرورة
وعن أَبي بردة، عن أَبي موسى الأشعري – رضي الله عنه -، قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – في غَزاةٍ وَنَحْنُ سِتَّةُ نَفَرٍ بَيْنَنَا بَعِيرٌ نَعْتَقِبُهُ، فَنقِبَت أقدَامُنَا وَنَقِبَت قَدَمِي، وسَقَطت أظْفَاري، فَكُنَّا نَلُفُّ عَلَى أرْجُلِنا الخِرَقَ، فَسُمِّيَت غَزْوَةَ ذَاتِ الرِّقَاعِ لِمَا كُنَّا نَعْصِبُ عَلَى أرْجُلِنَا مِنَ الخِرَقِ، قَالَ أَبُو بُردَة: فَحَدَّثَ أَبُو مُوسَى بِهَذَا الحَدِيثِ، ثُمَّ كَرِه ذَلِكَ، وقال: مَا كُنْتُ أصْنَعُ بِأنْ أذْكُرَهُ ! قَالَ: كأنَّهُ كَرِهَ أنْ يَكُونَ شَيْئاً مِنْ عَمَلِهِ أفْشَاهُ. متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Burdah amepokea kutoka kwa Abû Mûsâ al-Ash‘ary (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa amesema: “Tulitoka pamoja na Mtume ﷺ kwenda vitani, nasi tulikuwa kundi la watu sita, tulikuwa tuna ngamia tunaepishana kumpanda kwa zamu. Nyayo zetu zikawa laini (kwa sababu ya joto kali), hata unyayo wangu pia ukalainika na kucha zangu zikadondoka, tukawa tukijifunga vitambaa miguuni mwetu, ndio vikaitwa Vita vya Dhâturriqâ’ (Vita vya kujifunga Vitambaa) kwa sababu tulikuwa tukifunga vitambaa miguuni mwetu.” Abû Burdah anaeleza: “Abû Mûsâ akahadithia habari hii, kisha akachukia jambo hilo, na akasema: “Sikutenda hivyo kwa ajili ya kuzungumzia!” Kana kwamba amechukia kuwa ameidhihirisha amali yake.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim]]