0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

496. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Njaa, Maisha Ya Chini Kutosheka Kwa Vichache Katika Vyakula…..

 باب فضل الجوع وخشونة العيش والاقتصار عَلَى القليل من المأكول والمشروب والملبوس وغيرها من حظوظ النفس وترك الشهوات


وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: خرجَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – ذَاتَ يَوْمٍ أَوْ لَيْلَةٍ، فَإذَا هُوَ بأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ – رضي الله عنهما -، فَقَالَ: {مَا أخْرَجَكُمَا مِنْ بُيُوتِكُما هذِهِ السَّاعَةَ؟} قَالا: الجُوعُ يَا رسول الله. قَالَ: {وَأنَا، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لأخْرَجَنِي الَّذِي أخْرَجَكُما، قُوما} فقَامَا مَعَهُ، فَأتَى رَجُلاً مِنَ الأَنْصَارِ، فَإذَا هُوَ لَيْسَ في بيْتِهِ، فَلَمَّا رَأَتْهُ المَرْأَةُ، قالت: مَرْحَبَاً وَأهلاً. فقال لَهَا رسول الله – صلى الله عليه وسلم -:{أيْنَ فُلانُ؟} قالت: ذَهَبَ يَسْتَعْذِبُ لنَا المَاءَ. إِذْ جَاءَ الأَنْصَارِيُّ، فَنَظَرَ إِلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم – وَصَاحِبَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: الحَمْدُ للهِ، مَا أَحَدٌ الْيَوْمَ أكْرَمَ أضْيَافاً مِنِّي، فَانْطَلَقَ فَجَاءهُمْ بِعِذْقٍ فِيهِ بُسْرٌ وَتَمْرٌ وَرُطَبٌ، فَقَالَ: كُلُوا، وَأَخَذَ الْمُدْيَةَ، فَقَالَ لَهُ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -: {إيْاكَ وَالْحَلُوبَ} فَذَبَحَ لَهُمْ، فَأكَلُوا مِنَ الشَّاةِ وَمِنْ ذَلِكَ العِذْقِ وَشَرِبُوا. فَلَمَّا أنْ شَبِعُوا وَرَوُوا قَالَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – لأَبي بَكْر وَعُمَرَ – رضي الله عنهما -: {وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتُسْأَلُنَّ عَنْ هَذَا النَّعِيمِ يَوْمَ القِيَامَةِ، أَخْرَجَكُمْ مِنْ بُيُوتِكُمُ الْجُوعُ، ثُمَّ لَمْ تَرْجِعُوا حَتَّى أصَابَكُمْ هَذَا النَّعيمُ}       رواه مسلم.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ alitoka mchana fulani au usiku. Akakutana na Abûbakar na ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) , akawauliza: “Ni lipi lililowatoa majumbani mwenu wakati huu?” Wakajibu: “Ni njaa Yâ Rasûlallâh.” Akawaambia: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, nami pia lililonitoa ni kama lililowatoa, twendeni.” Wakafwatana naye hadi nyumbani kwa mtu miongoni mwa Ansari, lakini hawakumkuta nyumbani mwake. Mkewe (yule Asnari) alipomuona (Mtume) alimwambia: “Karibu na kongoni.” Mtume akamwuliza: “Yuwapi fulani?” Akamjibu: “Ameenda kututafutia maji-tamu.” Mara yule Ansari akaja. Akamtaza Mtume na Maswahaba zake, akasema: “Alhamdulillah! Leo hakuna mwenye wageni watukufu kama mimi!” Akaondoka na akarudi na kichala (kitawi cha matunda mengi yalio pamoja) cha tende tosa, tende kavu na tende mbivu. Akawaambia: “Kuleni.” Na akachukua kisu, Mtume akamwambia: “Usichinje mbuzi wa maziwa.” Akawachinjia, wakala mbuzi yule na katika kichala kile na wakanywa. Waliposhiba na wakamaliza kiu yao, Mtume ﷺ akawaambia Abûbakar na ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao): “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, mtaulizwa Siku ya Qiyama juu ya neema hii. Njaa imewatoa majumbani mwenu, kisha hamkurejea mpaka mkapata neema hii.”  
  [ Imepokewa na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.