باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر
وعن عبدِ الله بن مُغَفَّل – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رجل للنبي – صلى الله عليه وسلم -: يَا رسولَ الله، وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ، فَقَالَ: {انْظُرْ مَاذَا تَقُولُ؟} قَالَ: وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ، ثَلاَثَ مَرَّات، فَقَالَ: {إنْ كُنْتَ تُحِبُّنِي فَأَعِدَّ لِلْفَقْرِ تِجْفَافاً، فإنَّ الفَقْرَ أسْرَعُ إِلَى مَنْ يُحِبُّني مِنَ السَّيْلِ إِلَى مُنْتَهَاهُ} رواه الترمذي، وقال: {حديث حسن}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin Mughaffal (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Alikuja mtu hadi kwa Mtume ﷺ , akamwambia: “Yâ Rasûlallâh, (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu) Wallah mimi nakupenda!” Mtume ﷺ akamwambia: “Tazama unalosema!” Akasema: “Wallahi mimi nakupenda!” mara tatu. Akamwambia: “Ikiwa wanipenda kweli, basi jiandalie deraya ya ufukara, kwa hakika ufukara humfikia haraka yule anipendaye kuliko mafuriko ya maji kufikia yanapokomea.” [Imepokewa na Tirmidhy, na amesema: Hadîth hii ni Hasan.]