0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

47 DUA ANAYOISOMA MTU AKITOKEWA NA JAMBO ASILORIDHIA AU AKISHINDWA KUFANYA JAMBO

KINGA YA MUISLAMU

Amesema Mtume ﷺ [muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu  kuliko mumini dhaifu, na wote wana kheri.  Fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha na taka msaada kwa Mwenyezi Mungu   wala usichoke na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme “lau”  kama ningefanya kadha na kadha  yasingenitokea haya, lakini sema:

[ قدر الله وما شاء فعل ]

[Amepanga Mwenyezi Mungu  na analolitaka anafanya]

…… hakika neno la “lau”  linafungua matendo ya shetani’         [Imepokewa na Muslim.]

Hakika Mwenyezi Mungu  analaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo na ukishindwa na jambo kabisa sema:

[ حسبي الله ونعم الوكيل ]

[Mwenyezi Mungu  ananitosheleza, naye ni Mbora wa kutegemewa.]

SIKILIZA DUA HII 

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.