0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

464. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Kuipa Mgongo Dunia, Mahimizo Ya Kuwa Nao Kwa Uchache Na Fadhila Ya Ufukara.

باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر


وعن أَبي ذر – رضي الله عنه -، قَالَ: كُنْتُ أَمْشِي مَعَ النَّبي – صلى الله عليه وسلم – في حَرَّةٍ بِالمَدِينَةِ، فَاسْتَقْبَلَنَا أُحُدٌ، فقال: {يَا أَبَا ذَرٍّ} قلت: لَبَّيْكَ يَا رسولَ الله. فقال: {مَا يَسُرُّنِي أنَّ عِنْدِي مِثْلَ أُحُدٍ هَذَا ذَهَباً تَمْضي عَلَيَّ ثَلاَثَةُ أيّامٍ وَعِنْدِي مِنْهُ دِينَارٌ، إِلاَّ شَيْءٌ أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ، إِلاَّ أنْ أقُولَ بِهِ في عِبَادِ الله هكذا وَهَكَذَا وَهكَذَا} عن يَمِينِهِ وعن شِمَالِهِ وَمِنْ خَلْفِهِ، ثُمَّ سَارَ، فقال: {إنَّ الأَكْثَرينَ هُمُ الأَقَلُّونَ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلاَّ مَنْ قَالَ بالمَالِ هكَذَا وَهكَذَا وَهكَذَا} عن يمينِهِ وعن شِمَالِهِ وِمنْ خَلْفِهِ {وَقَلِيلٌ مَاهُمُ}. ثُمَّ قَالَ لي: {مَكَانَكَ لاَ تَبْرَحْ حَتَّى آتِيكَ} ثُمَّ انْطَلَقَ في سَوادِ اللَّيْلِ حَتَّى تَوَارَى، فَسَمِعْتُ صَوتاً، قَدِ ارْتَفَع، فَتَخَوَّفْتُ أنْ يَكُونَ أحَدٌ عَرَضَ للنَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم -، فَأرَدْتُ أنْ آتِيهِ فَذَكَرتُ قَوْله: {لا تَبْرَحْ حَتَّى آتِيَكَ} فلم أبْرَحْ حَتَّى أتَاني، فَقُلْتُ: لَقَدْ سَمِعْتُ صَوتاً تَخَوَّفْتُ مِنْهُ، فَذَكَرْتُ لَهُ، فقال: {وَهَلْ سَمِعْتَهُ؟} قلت: نَعَمْ، قَالَ: {ذَاكَ جِبريلُ أتَانِي. فقال: مَنْ مَاتَ مِنْ أُمَّتِكَ لاَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّةَ}، قلت: وَإنْ زَنَى وَإنْ سَرَقَ؟ قَالَ: {وَإنْ زَنَى وَإنْ سَرَقَ}  متفقٌ عَلَيْهِ، وهذا لفظ البخاري


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka Abû Dharri (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Nilikuwa nikitembea pamoja na Mtume ﷺ katika ardhi yenye mawe meusi Madina, mbele yetu tukakabiliwa na jabali la Uhud. Akaniita: “Ee Abû Dharri.” Nikamwitika: “Labeka Yâ Rasûlallâh.” Akasema: “Sipendezewi niwe na dhahabu mfani wa jabali hili la Uhud nipitiwe na siku tatu niwe nimebakiwa na dinari moja, ispokuwa labda nibaki na kitu nitakachokihifadhi kwa ajili ya kulipia deni, waila nitawapa waja wa Allâh hivi, hivi na hivi,” akaashiria kuliani, kushotoni na nyuma yake. Kisha akatembea. Akasema: “Hakika wenye mali nyingi ndio watakaokuwa na thawabu chache Siku ya Qiyama, ispokuwa aliefanya hivi, hivi na hivi, “ akaashiria kuliani, kushotoni na nyuma yake. Na ni wachache wanaofanya hivyo miongoni mwao. Kisha akaniambia: “Keti papo hapo usiondoke mpaka nitapokujia.” Akaondoka akaelekea kwenye giza la usiku mpaka akawa haonekani. Nikasikia sauti inapanda, nikachelea isije ikawa kuna mtu amemkaribia Mtume kwa ubaya. Nikataka nimwendee lakini nikakumbuka neno lake Usiondoke mpaka nitapokujia. Basi sikuondoka mpaka akanijia. Nikamwambia; Nimeisikia sauti hata nikaichelea. Akaniuliza: Na umeisikia? Nikamjibu: Ndio. Akaniambia: Huyo alikuwa ni Jibrîl, amenijia akaniambia: Atakayekufa katika umati wako ilihali hamshirikishi Allâh kwa chochote, ataingia Peponi. Nikamwuliza: Hata akizini na akiiba? Akanijibu: Hata akizini na akiiba.  [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.