0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

453. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Kulia Kwa Kumuogopa Mwenyezi Mungu Na Kuwa Na Shauku Ya Kukutana Naye.)

باب فضل البكاء من خشية الله تَعَالَى وشوقاً إِليه


وعن ابن عمر – رضي الله عنهما -، قَالَ: لَمَّا اشْتَدَّ برسول الله – صلى الله عليه وسلم – وَجَعُهُ، قِيلَ له في الصَّلاَةِ، فقال: {مُرُوا أَبَا بَكْرٍ فَلْيُصَلِّ بِالنَّاسِ} فقالت عائشة – رضي الله عنها -: إنَّ أَبَا بَكْرٍ رَجُلٌ رَقِيقٌ، إِذَا قَرَأَ القُرْآنَ غَلَبَهُ البُكَاءُ، فقال: {مُرُوهُ فَليُصَلِّ}

وفي رواية عن عائشة، – رضي الله عنها -، قالت: قلت: إنَّ أَبَا بَكْرٍ إِذَا قَامَ مَقَامَكَ لَمْ يُسْمِعِ النَّاسَ مِنَ البُكَاءِ.  متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka Abdullâh bin ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia: “Mtume alipozidiwa na maradhi yake, alijulishwa kuwa wakati wa Swala umefika. Akasema: [Mwamrisheni Abûbakar awaswalishe watu.] ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) akamwambia: “Hakika Abûbakar ana moyo laini, anaposoma Qur’âni huzidiwa na kilio.” Akasema: [ Mwamrisheni Abûbakar awaswalishe watu.]
Riwaya nyingine kutoka kwa ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) imesema: “Nikamwambia: “Hakika Abûbakar anaposimama makamu yako, watu huwa hawasikii kutokana na kilio.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim. ] 


Begin typing your search above and press return to search.