0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

446. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Kulia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuwa na Shauku ya kukutana naye.)

باب فضل البكاء من خشية الله تَعَالَى وشوقاً إِليه


وعن ابن مسعود – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ لِي النَّبيُّ – صلى الله عليه وسلم -: {اقْرَأْ عليَّ القُرْآنَ} قلت: يَا رسول اللهِ، أقرأُ عَلَيْكَ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ؟! قَالَ: {إِنِّي أُحِبُّ أنْ أسْمَعَهُ مِنْ غَيرِي} فَقَرَأْتُ عَلَيْهِ سورةَ النِّسَاءِ، حَتَّى جِئْتُ إِلى هذِهِ الآية: ﴿فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هؤُلاءِ شَهيداً﴾ [ النساء: 41 ] قَالَ: {حَسْبُكَ الآنَ} فَالَتَفَتُّ إِلَيْهِ فإذا عَيْنَاهُ تَذْرِفَان.   متفقٌ عَلَيْهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka Abdullâh bin Mas‘ûd (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Siku moja Mtume ﷺ aliniabia: “Nisomee Qur’âni.” Nikamwambia: “Yâ Rasûlallâh, (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu) nikusomee na ilihali imeteremshwa kwako?!” Akaniambia: “Mimi napenda kuisikia kwa mwenzangu.” Nikaanza kumsomea Sûratun-nisâ, mpaka nikafikia katika Aya hii: “Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa?” [4:41]. Akasema: “Sasa yatosha.” Nikamtazama, nikaona macho yake yanabubujika machozi.”]    [ Wameafikiana Bukhari na Muslim. ]


Begin typing your search above and press return to search.