0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

438. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kutaraji (Rehema Za Mwenyezi Mungu.)

باب الرجاء


وعن أَبي نجيح عمرو بن عَبَسَة – بفتح العين والباءِ – السُّلَمِيِّ – رضي الله عنه -، قَالَ: كُنْتُ وأنَا في الجاهِلِيَّةِ أظُنُّ أنَّ النَّاسَ عَلَى ضَلاَلَةٍ، وَأَنَّهُمْ لَيْسُوا عَلَى شَيْءٍ، وَهُمْ يَعْبُدُونَ الأَوْثَانَ، فَسَمِعْتُ بِرَجُلٍ بِمَكَّةَ يُخْبِرُ أخْبَاراً، فَقَعَدْتُ عَلَى رَاحِلَتِي، فَقَدِمْتُ عَلَيهِ، فإِذَا رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – مُسْتَخْفِياً، جرَءاءُ عَلَيهِ قَومُهُ، فَتَلَطَّفَتُ حَتَّى دَخَلْتُ عَلَيهِ بِمَكَّةَ، فَقُلْتُ لَهُ: مَا أنْتَ؟ قَالَ: {أنا نَبيٌّ} قُلْتُ: وما نبيٌّ؟ قَالَ: {أرْسَلَنِي الله} قُلْتُ: وبأيِّ شَيْء أرْسَلَكَ؟ قَالَ: {أَرْسَلَنِي بِصِلَةِ الأرْحَامِ، وَكَسْرِ الأَوْثَانِ، وَأنْ يُوَحَّدَ اللهُ لاَ يُشْرَكُ بِهِ شَيْء} قُلْتُ: فَمَنْ مَعَكَ عَلَى هَذَا؟ قَالَ: {حُرٌّ وَعَبْدٌ} ومعه يَوْمَئذٍ أَبُو بكرٍ وبلالٌ – رضي الله عنهما -، قُلْتُ: إنّي مُتَّبِعُكَ، قَالَ: {إنَّكَ لَنْ تَسْتَطيعَ ذلِكَ يَومَكَ هَذَا، ألا تَرَى حَالي وحالَ النَّاسِ؟ وَلَكِنِ ارْجعْ إِلَى أهْلِكَ فَإِذَا سَمِعْتَ بي قَدْ ظَهرْتُ فَأتِنِي} قَالَ: فَذَهَبْتُ إِلَى أهْلِي وقَدِمَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – المَدِينَةَ حَتَّى قَدِمَ نَفَرٌ مِنْ أهْلِي المَدِينَةَ، فقلتُ: مَا فَعَلَ هَذَا الرَّجُلُ الَّذِي قَدِمَ المَدِينَةَ؟ فقالوا: النَّاس إلَيهِ سِرَاعٌ، وَقَدْ أرادَ قَومُهُ قَتْلَهُ، فلَمْ يَسْتَطِيعُوا ذلِكَ، فقَدِمْتُ المدينَةَ، فَدَخَلْتُ عَلَيهِ، فقلتُ: يَا رَسُول الله أَتَعْرِفُني؟ قَالَ: {نَعَمْ، أنْتَ الَّذِي لَقَيْتَنِي بمكّةَ} قَالَ: فقلتُ: يَا رَسُول الله، أخْبِرنِي عَمَّا عَلَّمَكَ الله وأَجْهَلُهُ، أخْبِرْنِي عَنِ الصَّلاَةِ؟ قَالَ: {صَلِّ صَلاَةَ الصُّبْحِ، ثُمَّ اقْصُرْ عَنِ الصَّلاَةِ حَتَّى تَرْتَفِعَ الشَّمْسُ قِيدَ رُمْحٍ، فَإنَّهَا تَطْلُعُ حِينَ تَطلُعُ بَيْنَ قَرْنَيْ شَيطَان، وَحينَئذٍ يَسجُدُ لَهَا الكُفَّارُ، ثُمَّ صَلِّ فَإنَّ الصَلاَةَ مَشْهُودَةٌ([269]) مَحْضُورةٌ حَتَّى يَسْتَقِلَّ الظِّلُّ بالرُّمْحِ، ثُمَّ اقْصُرْ عَنِ الصَّلاةِ، فَإنَّهُ حينئذ تُسْجَرُ([270]) جَهَنَّمُ، فإذَا أقْبَلَ الفَيْءُ فَصَلِّ، فَإنَّ الصَّلاةَ مَشْهُودَةٌ مَحضُورَةٌ حَتَّى تُصَلِّي العصرَ، ثُمَّ اقْصرْ عَنِ الصَّلاةِ حَتَّى تَغْرُبَ الشَّمْسُ، فإنَّهَا تَغْرُبُ بينَ قَرْنَيْ شَيطانٍ، وَحِينَئذٍ يَسْجُدُ لَهَا الكُفّارُ} قَالَ: فقلتُ: يَا نَبيَّ الله، فالوضوءُ حدثني عَنْهُ؟ فَقَالَ: {مَا مِنْكُمْ رَجُلٌ يُقَرِّبُ وَضُوءهُ، فَيَتَمَضْمَضُ وَيسْتَنْشِقُ فَيَسْتَنْثِرُ، إلاَّ خَرَّتْ خَطَايَا وَجْهِهِ مِنْ أطْرَافِ لِحْيَتِهِ مَعَ المَاءِ، ثُمَّ يَغْسِلُ يديهِ إِلَى المِرفقَيْن، إلاَّ خَرَّتْ خَطَايَا يَدَيْهِ مِنْ أنَامِلِهِ مَعَ الماءِ، ثُمَّ يَمْسَحُ رَأسَهُ، إلاَّ خرّتْ خطايا رأسِهِ من أطْرَافِ شَعْرِهِ مَعَ الماءِ، ثُمَّ يغسل قدميه إِلَى الكعْبَيْنِ، إلاَّ خَرَّتْ خَطَايَا رِجلَيْهِ مِنْ أنَاملِهِ مَعَ الماءِ، فَإنْ هُوَ قَامَ فَصَلَّى، فَحَمِدَ الله تَعَالَى، وأثنى عَلَيهِ ومَجَّدَهُ بالَّذي هُوَ لَهُ أهْلٌ، وَفَرَّغَ قلبه للهِ تَعَالَى، إلاَّ انْصَرفَ مِنْ خَطِيئَتِهِ كهيئته يَومَ وَلَدتهُ أُمُّهُ}

فحدث عَمرُو بن عَبسَة بهذا الحديث أَبَا أُمَامَة صاحِب رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ لَهُ أَبُو أُمَامَة: يَا عَمْرُو بنُ عَبسَة، انْظُر مَا تقولُ ‍! في مقامٍ واحدٍ يُعْطَى هَذَا الرَّجُلُ؟ فَقَالَ عَمْرٌو: يَا أَبَا أُمَامَة، لقد كَبرَتْ سِنّي، وَرَقَّ عَظمِي، وَاقْتَرَبَ أجَلِي، وَمَا بِي حَاجَةٌ أنْ أكْذِبَ عَلَى اللهِ تَعَالَى، وَلا عَلَى رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، لَوْ لَمْ أسمعه مِنْ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، إلاَّ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَينِ أَوْ ثَلاثاً – حَتَّى عَدَّ سَبْعَ مَرَّات – مَا حَدَّثْتُ أبداً بِهِ، وَلكنِّي سمعتُهُ أكثَر من ذلِكَ. رواه مسلم

قوله: {جُرَءاءُ عَلَيهِ قَومُه} هُوَ بجيم مضمومة وبالمد عَلَى وزنِ عُلماءَ، أيْ: جَاسِرونَ مُستَطِيلُونَ غيرُ هائِبينَ، هذِهِ الرواية المشهورةُ، ورواه الحُمَيْدِيُّ وغيرُهُ {حِرَاءٌ} بكسر الحاء المهملة، وَقالَ: معناه غِضَابٌ ذَوُو غَمّ وهَمّ، قَدْ عِيلَ صَبرُهُمْ بِهِ، حَتَّى أثَّرَ في أجسامهم، من قولِهِم: حَرَى جسمهُ يَحْرَى، إِذَا نَقَصَ مِنْ ألمٍ أَوْ غَمٍّ ونحوهِ، والصَّحيحُ أنَّهُ بالجيمِ

قوله – صلى الله عليه وسلم -: {بَيْنَ قَرنَيْ شيطان} أيْ ناحيتي رأسِهِ والمرادُ التَّمْثيلُ، وَمعْنَاهُ: أنه حينئذٍ يَتَحرَّكُ الشَّيطَانُ وَشيعَتُهُ، وَيتَسَلَّطُونَ

وقوله: {يُقَرِّبُ وَضوءهُ} معناه يُحضِرُ الماءَ الَّذِي يَتَوضّأ بِهِ، وقوله: {إلاَّ خَرَّت خطايا} هُوَ بالخاءِ المعجمة: أيْ سقطت، ورواه بعضُهم {جَرَت} بالجيم، والصحيح بالخاءِ وَهُوَ رواية الجمهور. وقوله: {فينْتَثرُ} أيْ يَستخرجُ مَا في أنفهِ مِنْ أذىً والنَّثْرَةُ: طَرَفُ الأنْفِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka Abû Najîh, ‘Amru bin ‘Abasah as-Sulamy (Radhi za Allah ziwe juu yake) amehadithia: “Nilipokuwa katika zama za ujahiliya, nilikuwa nimeyakinisha kuwa watu wako katika upotevu, hawako katika haki, nao walikuwa wakiabudu vijimungu (masanamu). Nikamsikia mtu huko Makkah akielezea mambo makubwa, nikapanda mnyama wangu, nikamwendea, nikamuona Mtume ﷺ amejificha, jamaa zake wanamfanyia ujasiri (wa kumwambia maneno mabaya), nikaingia Makkah kwa polepole (kwa kujificha). Nikamwuliza: “Ni nani wewe?” Akanijibu: “Ni Nabii.” Nikamwuliza: “Nabii ni nani?” Akajibu: “Allâh Amenituma.” Nikamwuliza: “Amekutuma jambo gani?” Akajibu: “Amenituma kuunga kizazi (undugu/uhusiano), kuvunja vijimungu (masanamu) na Allâh apwekeshwe wala asishirikishwe kwa chochote.” Nikamwuliza: “Ni nani aliye pamoja nawe katika jambo hili?” Akanijibu: “Mwungwana na mtumwa.” Siku hizo alikuwa yuko pamoja na Abûbakar na Bilâl (Radhi za Allah ziwe juu yao). Nikamwambia: “Mimi nitadhihirisha Uislamu na nitakuwa pamoja nawe (Makkah).” Akaniambia: “Hakika wewe hutaweza kufanya hivyo kwa leo. Kwani huoni hali yangu na watu jinsi walivyo? Lakini, rejea kwa jamaa zako (ubaki na Uislamu wako), utaposikia nimekuwa mshindi, utanijia.” Nikaenda kwa jamaa zangu, na Mtume ﷺ akaenda Madina, na nilikuwa kwa jamaa zangu, nikawa nachunguza habari, na nikiwauliza watu alipohamia Madina, hata wakaja watu katika jamaa zangu kutoka Madina. Nikawauliza: “Mtu huyu amekuwaje alipohamia Madina?” Wakaniambia: “Watu wanamkimbilia, na jamaa zake walitaka kumwua lakini hawakuweza.” Nikaenda Madina. Nikamwuliza: “Yâ Rasûlallâh (Ewe Mtume wa Mungu), wanijua?” Akajibu: “Ndio, wewe ndiye uliekutana nami Makkah.” Nikamwambia: “Yâ Rasûlallâh, nieleze Aliyokufundisha Allâh mambo ambayo siyajui. Nieleze kuhusu Swala.” Akasema: “Swali Swala ya asubuhi, kisha utaketi usiswali mpaka jua litakapopanda kiasi cha mkuki (katika mtazamo wa macho), kwani jua linapochomoza huchomoza baina ya pembe za shetani (yaani shetani na kundi lake ndipo wanapoanza harakati zao), na wakati huo makafiri hulisujudia jua. Halafu uswali, hakika Swala ya wakati huu inashuhudiwa na kuhudhuriwa na Malaika mpaka kivuli kitakapopungua katika urefu wa mkuki. Kisha utaacha kuswali, kwani wakati huo Jahannam huchochewa. Kivuli kitaporefuka, utaswali kwani Swala inashuhudiwa na kuhudhuriwa na Malaika mpaka uswali alasiri, kisha utaacha kuswali mpaka jua lizame, wakati huo huzama baina ya pembe za shetani, na wakati huo makafiri hulisujudia.” Nikamwambia: “Yâ Nabiyyallâh, nieleze kuhusu udhu.” Akasema: “Yeyote miongoni mwenu anaekisogeza karibu chombo chake cha kutawadha, akasukutua, akapandisha maji puani na akayatoa, huanguka dhambi za usoni mwake, mdomoni mwake na tundu zake za pua. Kisha anapoosha uso wake kama alivyoamrishwa na Allâh, huanguka dhambi za usoni mwake katika ncha za ndevu zake pamoja na maji, kisha anapoosha mikono yake hadi katika viwiko, huanguka dhambi za mikononi mwake kutoka katika vidole vyake pamoja na maji, kisha anapopangusa kichwa chake, huanguka dhambi za kichwani mwake katika ncha za nywele zake pamoja na maji, kisha anapoosha miguu yake hadi katika vifundo, huanguka dhambi za miguuni mwake katika kucha zake pamoja na maji, ataposimama kuswali, akamhimidi Allâh, akamsifu na akamtukuza kwa Sifa Zake Anazostahiki, na moyo wake akaujaza fikra ya Allâh, basi ataondoka akiwa hana dhambi kama alivyokuwa siku alipozaliwa na mama yake.”

‘Amru bin ‘Abasah akamhadithia Abû Umâma Swahaba wa Mtume ﷺ , Hadîth hii. Abû Umâma akamwambia: “Ee ‘Amru bin ‘Abasah, tazama unachosema! Katika makamu mamoja mtu huweza akapewa mambo yote haya?” ‘Amru akamwambia: “Ee Abû Umâma, hakika umri wangu umekuwa mkubwa, mifupa yangu imedhoofika na mauti yangu yamekaribia, sina haja ya kumzulia uwongo Allâh wala Mtume Wake! Lau kama jambo hili nimemsikia Mtume ﷺ mara moja au mbili au tatu – akahesabu hadi mara saba – nisingalihadithia habari hii. Lakini nimemsikia (Mtume ﷺ ) akisema zaidi ya mara hizo.” [ Imepokewa na Muslim ]


Begin typing your search above and press return to search.