باب الرجاء
وعن ابن مسعود – رضي الله عنه -، قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – في قُبَّة نَحْوَاً مِنْ أربَعِينَ، فَقَالَ: {أتَرْضَونَ أنْ تَكُونُوا رُبُعَ أهْلِ الجَنَّةِ؟} قُلْنَا: نَعَمْ. قَالَ: {أتَرْضَوْنَ أنْ تَكُونُوا ثُلُثَ أهلِ الجَنَّةِ؟} قُلْنَا: نَعَمْ، قَالَ: {وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمّدٍ بيَدِهِ، إنِّي لأَرْجُو أنْ تَكُونُوا نِصْفَ أهْلِ الجَنَّةِ وذلك أنَّ الجنَّةَ لاَ يَدْخُلُهَا إلاَّ نَفْسٌ مُسْلِمَةٌ، ومَا أنْتُم في أهْلِ الشِّركِ إلاَّ كَالشَّعْرَةِ البَيْضَاءِ في جلدِ الثَّورِ الأَسْوَدِ، أَوْ كَالشَّعْرَةِ السَّودَاءِ في جلدِ الثَّورِ الأحْمَر} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka ‘Abdullâh bin Mas‘ûd (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Tulikuwa pamoja na Mtume ﷺ katika hema takriban watu arubaini. Akatuuliza: “Mnaridhika muwe ndio robo ya watu wa Peponi?” Tukamjibu: “Ndio.” Akatuuliza tena: “Mnaridhika muwe ndio thuluthi ya watu wa Peponi?” Tukasema: “Ndio.” Akasema: [ Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake, mimi natarajia nyinyi mtakuwa ni nusu ya watu wa Peponi, kwa sababu hakuna atakayeingia Peponi ila Muislamu (aliejisalimisha kwa Allâh). Nanyi mkilinganishwa na mushrikina, ni kama unywele mweupe katika ngozi ya ng’ombe mweusi, au ni kama unywele mweusi katika ngozi ya ng’ombe mwekundu.] [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ]