0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

43 DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI KATIKA SWALA YAKE AU KISOMO CHAKE

KINGA YA MUISLAMU

 أعوذ بالله من الشيطان الرجيم واتفل على يسارك ]   ثلاثاً]

 مسلم 4/1729

[Najilinda na Mwenyezi Mungu   kutokana na shetani aliyelaaniwa]

Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu.

Imepokelewa kutoka kwa Uthman Ibn Al-Ass Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: [Nilimwambia Mtume ﷺ Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika shetani amenikalia kati yangu na kati ya swala yangu na kisomo changu, ananitatiza.  Akasema Mtume ﷺ [Huyo ni shetani aitwae “Khanzab” ukimuhisi amekujia basi muombe hifadhi Mwenyezi Mungu nae, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu]

……nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu  akaniondoshea.    [Imepokewa na Muslim.]

DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI 

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.