0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

420. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kutaraji (Rehema Za Mwenyezi Mungu.)

باب الرجاء


 وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {جَعَلَ الله الرَّحْمَةَ مِئَةَ جُزْءٍ، فَأمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ، وَأنْزَلَ في الأرْضِ جُزْءاً وَاحِداً، فَمِنْ ذلِكَ الجُزءِ يَتَرَاحَمُ الخَلائِقُ، حَتَّى تَرْفَعَ الدَّابّةُ حَافِرهَا عَنْ وَلَدِهَا خَشْيَةَ أنْ تُصِيبَهُ}

وفي رواية: {إنّ للهِ تَعَالَى مئَةَ رَحمَةٍ، أنْزَلَ مِنْهَا رَحْمَةً وَاحِدَةً بَيْنَ الجنِّ وَالإنس وَالبهائِمِ وَالهَوامّ، فبها يَتَعاطَفُونَ، وبِهَا يَتَرَاحَمُونَ، وبِهَا تَعْطِفُ الوَحْشُ عَلَى وَلَدِهَا، وَأخَّرَ اللهُ تَعَالَى تِسْعاً وَتِسْعينَ رَحْمَةً يرْحَمُ بِهَا عِبَادَهُ يَوْمَ القِيَامَة}          مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

ورواه مسلم أيضاً مِنْ رواية سَلْمَانَ الفارِسيِّ – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {إنَّ للهِ تَعَالَى مِئَة رَحْمَةٍ فَمِنْهَا رَحْمَةٌ يَتَرَاحمُ بِهَا الخَلْقُ بَيْنَهُمْ، وَتِسْعٌ وَتِسعُونَ لِيَومِ القِيَامَةِ}

وفي رواية: {إنَّ الله تَعَالَى خَلَقَ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاواتِ وَالأَرْضَ مَئَةَ رَحْمَةٍ كُلُّ رَحْمَةٍ طِبَاقُ مَا بَيْنَ السَّماءِ إِلَى الأرْضِ، فَجَعَلَ مِنْهَا في الأرضِ رَحْمَةً فَبِهَا تَعْطفُ الوَالِدَةُ عَلَى وَلَدِهَا، وَالوَحْشُ وَالطَّيْرُ بَعْضُهَا عَلَى بَعْض، فَإذا كَانَ يَوْمُ القِيَامَةِ أكملَهَا بِهذِهِ الرَّحمَةِ}


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimsikia Mtume   akisema: “Allâh Ameijaalia rehema ni sehemu mia, Akazizuwia sehemu tisaini na tisa Kwake, Akateremsha ardhini sehemu moja tu, katika sehemu hiyo (moja) viumbe wanarehemeana hata mnyama huinua mguu wake kumwondolea mtoto wake kwa kuchelea asije akamwumiza.

Riwaya nyingine imesema: Hakika Allâh Anazo rehema mia, katika hizo Ameteremsha moja tu miongoni mwa majini, wanadamu, wanyama na wadudu. Kwa rehema hiyo wanasaidiana, wanarehemeana na wanyama huwasaidia watoto wao. Na Allâh Ameziweka rehema (nyingine) tisaini na tisa Atakazowarehemu kwazo waja Wake Siku ya Qiyama.   [Wameafikiana Bukhari na Muslim]

Vile vile Muslim ameipokea Hadîth hii kwa mapokeo ya Salmân al-Fârisy (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume amesema: “Allâh Mtukufu Anazo rehema mia, katika rehema hizo kuna rehema (moja) ambayo viumbe wanarehemeana kwayo, na rehema nyingine tisaini na tisa zimeekwa kwa ajili ya Siku ya Qiyama.”

Riwaya nyingine imesema: Hakika Allâh Mtukufu Aliumba siku Aliyoumba mbingu na ardhi rehema mia (moja), kila rehema moja ina uwezo wa kujaza mbingu na ardhi. Akajaalia katika rehema hiyo iwe ardhini, kwa rehema hiyo mama anamhurumia mwanaye, mnyama na ndege wanahurumiana wao kwa wao. Itapokuwa Siku ya Qiyama, Allâh Atazikamilsha rehema zote kwa rehema hii.


Begin typing your search above and press return to search.