باب الرجاء
وعن عمر بن الخطاب – رضي الله عنه -، قَالَ: قدِم رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – بسَبْيٍ فَإِذَا امْرَأةٌ مِنَ السَّبْيِ تَسْعَى، إِذْ وَجَدَتْ صَبياً في السَّبْيِ أخَذَتْهُ فَألْزَقَتهُ بِبَطْنِهَا فَأَرضَعَتْهُ، فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {أتَرَوْنَ هذِهِ المَرْأةَ طَارِحَةً وَلَدَها في النَّارِ؟} قُلْنَا: لاَ وَاللهِ. فَقَالَ: {للهُ أرْحَمُ بِعِبَادِهِ مِنْ هذِهِ بِوَلَدِهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Umar bin al-Khattâb (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ alikuja na mateka, mwanamke mmoja katika mateka wale alikuwa akikimbia huku na kule, mara akamuona mtoto wa kimateka, akamchukua na akamwambatisha katika tumbo lake, akamnyonyesha. Mtume ﷺ akasema: “Mnadhani kuwa mwanamke huyu anaweza kumwingiza mwanaye motoni?” Tukajibu: “Hapana.” Akasema: “Mwenyezi Mungu ni Mrehemevu zaidi kwa waja Wake kuliko mwanamke huyu kwa mwanawe.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]