0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

417. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kutaraji (Rehema Za Mwenyezi Mungu.)

باب الرجاء


وعن عِتْبَانَ بن مالك – رضي الله عنه – وَهُوَ مِمَّن شَهِدَ بَدراً، قَالَ: كنت أُصَلِّي لِقَوْمِي بَني سَالِم، وَكَانَ يَحُولُ بَيْنِي وبَيْنَهُمْ وَادٍ إِذَا جَاءتِ الأَمْطَار، فَيَشُقُّ عَلَيَّ اجْتِيَازُهُ قِبَلَ مسْجِدِهم، فَجِئتُ رسولَ الله – صلى الله عليه وسلم – فقلت لَهُ: إنّي أنْكَرْتُ بَصَرِي وَإنَّ الوَادِي الَّذِي بَيْنِي وبَيْنَ قَومِي يَسيلُ إِذَا جَاءتِ الأمْطَارُ فَيَشُقُّ عَلَيَّ اجْتِيَازُهُ فَوَدِدْتُ أنَّكَ تَأتِي فَتُصَلِّي في بَيْتِي مَكَاناً أتَّخِذُهُ مُصَلّى، فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {سَأفْعَلُ} فَغَدَا رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – وَأَبُو بكر – رضي الله عنه – بَعْدَ مَا اشْتَدَّ النَّهَارُ، وَاسْتَأذَنَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – فَأذِنْتُ لَهُ، فَلَمْ يَجْلِسْ حَتَّى قَالَ: {أيْنَ تُحِبُّ أنْ أُصَلِّيَ مِنْ بَيْتِكَ؟} فَأشَرْتُ لَهُ إِلَى المَكَانِ الَّذِي أُحبُّ أنْ يُصَلِّيَ فِيهِ، فَقَامَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – فَكَبَّرَ وَصَفَفْنَا وَرَاءَهُ فَصَلَّى رَكعَتَينِ ثُمَّ سَلَّمَ وَسَلَّمْنَا حِينَ سَلَّمَ فَحَبَسْتُهُ عَلَى خَزيرَةٍ تُصْنَعُ لَهُ، فَسَمِعَ أهلُ الدَّارِ أنَّ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – في بَيْتِي فَثَابَ رِجالٌ مِنْهُمْ حَتَّى كَثُرَ الرِّجَالُ في البَيْتِ، فَقَالَ رَجُلٌ: مَا فَعَلَ مَالِكٌ لا أرَاهُ ! فَقَالَ رَجُلٌ: ذلِكَ مُنَافِقٌ لا يُحِبُّ الله ورسولَهُ، فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {لا تَقُلْ ذلِكَ، ألاَ تَرَاهُ قَالَ: لا إلهَ إلاَّ الله يَبْتَغي بذَلِكَ وَجهَ الله تَعَالَى} فَقَالَ: اللهُ ورسُولُهُ أعْلَمُ أمَّا نَحْنُ فَوَاللهِ مَا نَرَى وُدَّهُ وَلاَ حَدِيثَهُ إلاَّ إِلَى المُنَافِقينَ ! فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {فإنَّ الله قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ: لا إلهَ إلاَّ الله يَبْتَغِي بذَلِكَ وَجْهَ الله}    مُتَّفَقٌ عَلَيهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى




Imepokewa kutoka kwa‘Itbân bin Mâlik (Radhi za Allah ziwe juu yake) – ambaye ni katika waliohudhuria Vita vya Badr – amesimulia: “Nilikuwa nikiwaswalisha jamaa zangu Banî Sulaim. Ilikuwa nikikatizwa na maji ya mvua inaponyesha, maji hayo huwa yakikaa katika jangwa lililokuwa baina yangu na wao, hapo ikawa uzito kwangu kulivuka jangwa hilo kuelekea katika Msikiti wao. Nikamwendea Mtume , nikamwambia: “Macho yangu yamedhoofika, na jangwa liliopo baina yangu na jamaa zangu huwa likimiminika maji mvua zinaponysha, hapo ikawa uzito kwangu kulivuka. Basi ningependelea uje uswali nyumbani mwangu mahala ambapo nitapafanya ndipo pa kuswalia.” Mtume akamwambia: “Nitafanya.” Mtume akaja kwangu pamoja na Abûbakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakati wa mchana. Mtume akapiga hodi (ya kuingia nyumbani), nikamruhusu, alipoingia hakuketi bali aliuliza: “Ni sehemu ipi unayopenda niswali nyumbani mwako?” Nikamwashiria mahala ninapopapenda aswali. Mtume  akasimama, akabipa Takbîr, nasi tukapanga safu nyuma yake, akaswali rakaa mbili, kisha akapiga salamu, nasi tukatoa salamu alipotoa salamu. Nikamzuwia kwa ajili ya dhifa ya khazîra (unga unaopikwa kwa mafuta) iliotengenezwa kwa ajili yake. Watu wa sehemu ile wakasikia kuwa Mtume yuko nyumbani mwangu, basi watu wakamiminika hata wakajaa nyumbani. Mtu mmoja akauliza: “Mâlik ana nini mbona simuoni!? Mtu mwingine akasema: “Huyo ni mnafiki hampendi Allâh na Mtume Wake.” Mtume akamwambia: “Usiseme hivyo, kwani humjui kuwa yeye amesema Lâ-ilâha illallâh akitaka Radhi ya Allâh kwa kusema huko?” Akasema: “Allâh na Mtume Wake Wanajua. Ama sisi Wallahi tunamuona mapenzi yake na mazungumzo yake daima huwa ni kwa wanafiki!” Mtume akasema: “Hakika Allâh Amemharamishia kuingia motoni kila aliesema Lâ-ilâha illallâh akitafuta Radhi ya Allâh kwa kusema huko.                       [ Wameafikiana na Bukhari na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.