باب الرجاء
وعن أنس – رضي الله عنه -: أن النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم – ومعاذ رديفه عَلَى الرَّحْل، قَالَ: {يَا مُعَاذُ} قَالَ: لَبِّيْكَ يَا رَسُول الله وَسَعْدَيْكَ، قَالَ: {يَا مُعَاذُ} قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُول الله وَسَعْدَيْكَ، قَالَ: {يَا مُعَاذُ} قَالَ: لَبِّيْكَ يَا رَسُول الله وسَعْدَيْكَ، ثَلاثاً، قَالَ: {مَا مِنْ عَبْدٍ يَشْهَدُ أن لا إلهَ إلاَّ الله، وَأنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ صِدْقاً مِنْ قَلْبِهِ إلاَّ حَرَّمَهُ الله عَلَى النَّار} قَالَ: يَا رَسُول الله، أفَلاَ أخْبِرُ بِهَا النَّاس فَيَسْتَبْشِروا؟ قَالَ: {إِذاً يَتَّكِلُوا} فأخبر بِهَا مُعاذٌ عِنْدَ موتِه تَأثُّماً. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وقوله: {تأثُّماً} أي خوفاً مِنْ الإثم في كَتْم هَذَا العلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Alikuwa Mu‘âdh amepanda nyuma ya punda wa Mtume ﷺ. Akamwita: “Ewe Mu‘âdh.” Akamwitika: “Labbaika Yâ Rasûlallâh wa sadaika (nakuitika na kuitii amri yako ewe Mtume), Akamwita tena: “Ewe Muâdh.” Akamwitika: “Labbaika Yâ Rasûlallâh wa sadaika (nakuitika na kuitii amri yako ewe Mtume) Akamwita tena mara ya tatu: “Ewe Muâdh. “ Akamwitika: “Labbaika Yâ Rasûlallâh wa sadaika (nakuitika na kuitii amri yako ewe Mtume). Akasema: [ Mja yeyote anaeshuhudia kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allâh na kuwa Muhammad ni Mtume wa Allâh ilihali ya kusadikisha kweli moyoni mwake, Allâh Atamharamishia kuingia motoni. ] Akasema: Yâ Rasûlallâh, waonaje niwaeleze watu ili wapokee bishara njema? Akamwambia: Ukiwaambia wataacha kufanya amali. Muâdh akaiyeleza habari hii alipokaribia kufa kwa kuchelea asije akapata dhambi (ya kuficha ilimu).] [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]