باب الخوف
وعن عائشة – رضي الله عنها -، قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ القِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلاً} قُلْتُ: يَا رَسُول الله، الرِّجَالُ وَالنِّساءُ جَمِيعاً يَنْظُرُ بَعضُهُمْ إِلَى بَعْض؟! قَالَ: {يَا عائِشَةُ، الأمرُ أشَدُّ مِنْ أنْ يُهِمَّهُمْ ذلِكَ}
وفي رواية: {الأَمْرُ أهمُّ مِنْ أنْ يَنْظُرَ بَعضُهُمْ إِلَى بَعض} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: [ Watu watafufuliwa Siku ya Qiyama ilihali hawana viatu, wako uchi ni mazunga (hawakutahiriwa).” Nikamwuliza: ] Yâ Rasûlallâh, (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu) wanaume na wanawake wote watatazamana?!” Akaniambia: [Ee Âisha, hali itakuwa ngumu sana hata hawataweza kushughulika na jambo hilo!]
Riwaya nyingine imesema: [Hali itakuwa ngumu mno hata hawataweza kutazamana!]
[ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]