باب الخوف
وعن النعمان بن بشير – رضي الله عنهما -، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {إنَّ أهْوَنَ أهْلِ النَّارِ عَذَاباً يَوْمَ القِيَامَةِ لَرَجُلٌ يوضعُ في أخْمَصِ قَدَمَيْهِ جَمْرَتَانِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ. مَا يَرَى أنَّ أَحَداً أشَدُّ مِنْهُ عَذَاباً، وَأنَّهُ لأَهْوَنُهُمْ عَذَاباً} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Nu’mân bin Bashîr (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Hakika atakayekuwa na adhabu ndogo mno katika watu wa motoni Siku ya Qiyama ni mtu atakayeekewa katika vishimo vya nyayo zake makaa mawili (ya moto) ilihali ubongo wake unatokota, atadhani kuwa hakuna mwenye adhabu kali kama yake, na kwa hakika mtu huyo ndiye mwenye adhabu ndogo zaidi (kuliko wote)! ] [ Wameafikiana Bukhari na Muslim. ]