0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

394. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwachukulia Watu Kwa Dhahiri Yao Na Siri Zao Kumuachia Allah

باب إجراء أحكام الناس عَلَى الظاهر وسرائرهم إِلَى الله تَعَالَى


وعن جندب بن عبد الله – رضي الله عنه -: أنَّ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – بَعَثَ بَعْثاً مِنَ المُسْلِمينَ إِلَى قَومٍ مِنَ المُشرِكينَ، وَأنَّهُمْ التَقَوْا، فَكَانَ رَجُلٌ مِنَ المُشْركينَ إِذَا شَاءَ أنْ يَقْصِدَ إِلَى رَجُل مِنَ المُسْلِمينَ قَصَدَ لَهُ فَقَتَلَهُ، وَأنَّ رَجُلاً مِنَ المُسْلِمِينَ قَصَدَ غَفْلَتَهُ. وَكُنَّا نتحَدَّثُ أنَّهُ أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ، فَلَمَّا رَفَعَ عَلَيهِ السَّيفَ، قَالَ: لا إلهَ إلاَّ اللهُ، فَقَتَلهُ، فَجَاءَ البَشيرُ إِلَى رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – فَسَألَهُ وَأخبَرَهُ، حَتَّى أخْبَرَهُ خَبَرَ الرَّجُلِ كَيْفَ صَنَعَ، فَدَعَاهُ فَسَألَهُ، فَقَالَ: {لِمَ قَتَلْتَهُ؟} فَقَالَ: يَا رَسُول اللهِ، أوْجَعَ في المُسلِمِينَ، وَقَتَلَ فُلاناً وفلاناً، وسمى لَهُ نَفراً، وَإنِّي حَمَلْتُ عَلَيهِ، فَلَمَّا رَأى  السَّيفَ، قَالَ: لا إلهَ إلاَّ اللهُ. قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -:  {أقَتَلْتَهُ؟} قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: {فَكَيفَ تَصْنَعُ بلاَ إلهَ إلاَّ اللهُ، إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ؟} قَالَ: يَا رَسُول الله، اسْتَغْفِرْ لِي. قَالَ: {وكَيفَ تَصْنَعُ بِلا إلهَ إلاَّ الله إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ؟} فَجَعَلَ لاَ يَزِيدُ عَلَى أنْ يَقُولَ: {كَيفَ تَصْنَعُ بِلا إلهَ إلاَّ الله إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ}    رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Jundub bin ‘Abdullâh (Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia kuwa, Mtume alituma jeshi la Waislamu kwenda kwa mushrikina. Wakapambana. Ikawa mtu miongoni mwa mushrikina anapotaka kumuuwa mtu miongoni mwa Waislamu, humvizia na akamwuuwa. Mtu mmoja katika Waislamu, akamuotea akiwa ameghafilika, tulikuwa tukisema mtu mwenyewe alikuwa ni Usâma bin Zaid. Alipouwinua upanga, yule mtu alisema “Lâ-ilâha illallâh,” yeye (Usâma) akamuuwa. Mpelekaji bishara alipoenda kwa Mtume (Mtume) alimwuliza, yule mbashiri akamweleza (habari zote) mpaka akamweleza habari ya yule mtu jinsi alivyofanya. Akamwita Usâma na akamwuliza: “Mbona ulimuuwa?” Akajibu: “Yâ Rasûlallâh, aliwaumiza Waislamu na akamuuwa fulani na fulani – akawataja watu kadhaa – nami nikamshambulia, alipouwona upanga alisema Lâ-ilâha illallâh.” Mtume akamwuliza: “Ulimuuwa?” Akajibu: “Ndio.” Akamwuliza: “Utaifanyia nini Lâ-ilâha illallâh itakapokuja Siku ya Qiyama?” (Usâma) akasema: “Yâ Rasûlallâh, niombee maghfira!” Mtume akamwuliza: “Utaifanyia nini Lâ-ilâha illallâh itakapokuja Siku ya Qiyama?” Akawa hazidi neno zaidi ya kusema: [Utaifanyia nini Lâ-ilâha illallâh itakapokuja Siku ya Qiyama?]  [ Imepokewa na Muslim. ]


Begin typing your search above and press return to search.