باب إجراء أحكام الناس عَلَى الظاهر وسرائرهم إِلَى الله تَعَالَى
وعن أَبي معبد المقداد بن الأسْود – رضي الله عنه -، قَالَ: قُلْتُ لرسول الله – صلى الله عليه وسلم -: أرَأيْتَ إنْ لَقِيتُ رَجُلاً مِنَ الكُفَّارِ، فَاقْتتَلْنَا، فَضَرَبَ إحْدَى يَدَيَّ بِالسَّيْفِ، فَقَطَعَها، ثُمَّ لاذَ مِنِّي بِشَجَرَةٍ، فَقَالَ: أسْلَمْتُ لِلهِ، أأقْتُلُهُ يَا رَسُول الله بَعْدَ أنْ قَالَهَا؟ فَقَالَ: {لا تَقْتُلهُ} فَقُلْتُ: يَا رَسُول الله، قَطَعَ إحْدَى يَدَيَّ، ثُمَّ قَالَ ذلِكَ بَعْدَ مَا قَطَعَهَا؟! فَقَالَ: {لا تَقتُلْهُ، فإنْ قَتَلْتَهُ فَإنَّهُ بِمَنْزِلَتِكَ قَبْلَ أنْ تَقْتُلَهُ، وَإنَّكَ بِمَنْزِلَتِهِ قَبْلَ أنْ يَقُولَ كَلِمَتَهُ التي قَالَ} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Ma’bad, al-Miqdâd bin al-‘Aswad Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: [ Nilimwuliza Mtume ﷺ : “Niambie, lau nitakutana na mtu katika makafiri, tukapigana, akaukata mkono wangu kwa upanga, halafu akajikinga nami kwa mti na akasema: “Nimesilimu kwa ajili ya Allâh,” je, nimuuwe Yâ Rasûlallâh baada ya kuwa ameshasema neno hilo? Akajibu: Usimwuuwe. Nikamwuliza: Yâ Rasûlallâh, ameukata mkono wangu, kisha akasema hivyo baada ya kuwa ameshaukata? Akasema: Usimwuuwe. Utakapomwuuwa, yeye atakuwa katika daraja yako kabla ya kumwuuwa, nawe utakuwa katika daraja yake kabla yeye hajasema neno lake alilosema.] [ Wameafikiana Bukhari na Muslim. ]