0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

382. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwatembelea Watu Wa Kheri, Kuketi Nao,Kusuhubina Nao, Kuwapenda Na Kuomba Kutembelewa Nao….

 باب فضل الحب في الله والحث عَلَيهِ وإعلام الرجل من يحبه، أنه يحبه، وماذا يقول لَهُ إِذَا أعلمه


وعن أَبي إدريس الخولاني رحمه الله، قَالَ:دخَلْتُ مَسْجِدَ دِمَشْقَ، فَإذَا فَتَىً بَرَّاق الثَّنَايَا وَإِذَا النَّاسُ مَعَهُ، فَإِذَا اخْتَلَفُوا في شَيْءٍ، أَسْنَدُوهُ إِلَيْه، وَصَدَرُوا عَنْ رَأيِهِ، فَسَأَلْتُ عَنْهُ، فَقيلَ: هَذَا مُعَاذُ بْنُ جَبَل – رضي الله عنه -. فَلَمَّا كَانَ مِنَ الغَدِ، هَجَّرْتُ، فَوَجَدْتُهُ قَدْ سَبَقَنِي بالتَّهْجِيرِ، ووَجَدْتُهُ يُصَلِّي، فانْتَظَرتُهُ حَتَّى قَضَى صَلاتَهُ، ثُمَّ جِئْتُهُ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ، فَسَلَّمْتُ عَلَيهِ، ثُمَّ قُلْتُ: وَاللهِ إنّي لأَحِبُّكَ لِله، فَقَالَ: آلله؟ فَقُلْتُ: اللهِ، فَقَالَ: آللهِ؟ فَقُلْتُ: اللهِ، فَأخَذَنِي بِحَبْوَةِ رِدَائِي، فجبذني إِلَيْهِ، فَقَالَ: أبْشِرْ ! فإنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ الله – صلى الله عليه وسلم -، يقول: {قَالَ الله تَعَالَى: وَجَبَتْ مَحَبَّتي لِلْمُتَحابين فيَّ، وَالمُتَجَالِسينَ فيَّ، وَالمُتَزَاوِرِينَ فيَّ، وَالمُتَبَاذِلِينَ  فِيَّ}  حديث صحيح رواه مالك في الموطأ بإسناده الصحيح

قوله: {هَجَّرْتُ} أيْ بَكَّرْتُ، وَهُوَ بتشديد الجيم قوله: {آلله فَقُلْت: الله} الأول بهمزة ممدودة للاستفهام، والثاني بلا مد


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abû Idrîs al-Khawlâny (Mungu amrahamu) amesimulia: “Niliingia katika Msikiti wa Dimashqi, mara nikamuona kijana mwenye meno ya kung’aa (mwingi wa tabasamu) na watu wameketi pamoja naye, wanapohitilafiana katika jambo humuuliza na wakaichukua rai yake. Nikamwulizia, nikaambiwa kuwa huyu ni Mu‘âdh bin Jabal. Ilipofika siku ya pili yake nilirauka, nikamkuta kuwa amenitangulia kurauka, nikamkuta anaswali, nikamsubiri mpaka akamaliza kuswali. Kisha nikamwendea kwa upande wa usoni mwake, nikamsalimia na nikamwambia: Wallahi mimi nakupenda kwa ajili ya Allâh. Akaniuliza: “Wallahi?” Nikamjibu: “Wallahi.” Akaniuliza tena: “Wallahi?” Nikamjibu: “Wallahi.” Akaishika nguo yangu katikati ya kitovu changu, akanivutia kwake na akaniambia: “Pokea bishara! Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Allâh Mtukufu Amesema: “Mapenzi Yangu yamewapasa waliopendana kwa ajili Yangu, walioketi kwa ajili Yangu, wanaotembeleana kwa ajili Yangu na wanaosaidiana kwa ajili Yangu.”                   [ Imepokewa na Mâlik katika al-Muwatta. Isnadi yake ni Sahîh.]


Begin typing your search above and press return to search.