باب زيارة أهل الخير ومجالستهم وصحبتهم ومحبتهم وطلب زيارتهم والدعاء منهم وزيارة المواضع الفاضلة
وعن أُسَير بن عمرو ويقال”: ابن جابر وهو ”بضم الهمزة وفتح السين المهملة” قال: كان عمر بن الخطاب إذا أتى عليه أمداد أهل اليمن سألهم: أفيكم أويس بن عامر؟ حتى أتى على أويس رضي الله عنه ، فقال له: أنت أويس بن عامر؟ قال: نعم، قال: من مراد ثم من قرن؟ قال: نعم قال: فكان بك برص، فبرأت منه إلا موضع درهم؟ قال نعم قال: لك والدة؟ قال نعم، قال : سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول ”يأتي عليكم أويس بن عامر مع أمداد أهل اليمن من مراد، ثم من قرن كان به برص، فبرأ منه إلا موضع درهم، له والدة هو بها بر لو أقسم على الله لأبره، فإن استطعت أن يستغفر لك فافعل” فاستغفر لي فاستغفر له، فقال له عمر: أين تريد؟ قال: الكوفة، قال: ألا أكتب لك إلى عاملها؟ قال: أكون في غبراء الناس أحب إلي، فلما كان من العام المقبل حج رجل من أشرافهم، فوافق عمر، فسأله عن أويس، فقال: تركته رث البيت قليل المتاع، قال: سمعت رسول الله يقول: يأتي عليكم أويس بن عامر مع أمداد من أهل اليمن من مراد ، ثم من قرن، كان به برص فبرأ منه إلا موضع درهم، له والدة هو بها بر لو أقسم على الله لأبره، فإن استطعت أن يستغفر لك : فافعل، فأتى أويسًا، فقال استغفر لي قال: أنت أحدث عهدًا بسفر صالح، فاستغفر لي. قال: لقيت عمر؟ قال: نعم، فاستغفر له، ففطن له الناس، فانطلق على وجهه. (رواه مسلم).
وفي رواية لمسلم أيضًا عن أُسِير بن جابر رضي الله عنه أن أهل الكوفة وفدوا على عمر رضي الله عنه ، وفيهم رجل ممن كان يسخر بأويس، فقال عمر: هل هاهنا أحد من القرنين؟ فجاء ذلك الرجل، فقال عمر: إن رسول الله صلى الله عليه وسلم قد قال: “إن رجلا يأتيكم من اليمن يقال له : أويس، لا يدع باليمن غير أم له، قد كان به بياض فدعا الله تعالى، فأذهبه إلا موضع الدينار أو الدرهم ، فمن لقيه منكم، فليستغفر لكم”.
وفي رواية له عن عمر رضي الله عنه قال: ”إنى سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ”إن خير التابعين رجل يقال له: أويس: وله والدة وكان به بياض، فمروه، فليستغفر لكم”.
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Usair bin ‘Amri – pia ajulikana kwa jina la Ibnu Jâbir, amesimulia: “Umar bin al-Khattâb Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa anapotembelewa na makundi ya watu wa Yemen huwauliza: “Miongoni mwenu yuko Uwais bin ‘Âmir?” Safari moja akakutana na Uwais bin ‘Âmir Radhi za Allah ziwe juu yake , akamwuliza: “Wewe ndiye Uwais bin ‘Âmir?” Akamjibu: “Ndio.” Akamwuliza: “Unatoka katika kabila la Murâd ukoo wa Qarni?” Akajibu: “Ndio.” Akamwuliza: “Ulikuwa una mbalanga, ukapona ela mahala padogo sawa na (mzunguko wa) dirhamu?” Akajibu: “Ndio.” Akamwuliza: “Unaye mama?” Akamjibu: “Ndio.” Akamwambia: “Nimemsikia Mtume ﷺ akisema: “Mutajiwa na Uwais bin ‘Âmir pamoja na makundi ya watu wa Yemen anaetoka katika kabila la Murâd kisha kutoka katika ukoo wa Qarni. Alikuwa ana mbalanga, akapona ela mahala kama dirhamu tu, ana mama anayemfanyia hisani kubwa. Lau atamwapia Allâh (ili Amfanyie jambo) basi Angalimfanyia. Ukiweza kumwambia akuombee maghfira, basi fanya hivyo.” Basi niombee maghfira.” Akamwombea maghfira. ‘Umar akamwuliza: “Unaelekea wapi?” Akamjibu: “al-Kûfah (‘Iraq).” Akamwambia: “Waonaje nikupe barua umpelekee Amiri wa al-Kûfah?” Akamwambia: “Napendelea zaidi kuwa pamoja na watu masikini wasiojulikana.” Ulipofika mwaka uliofwatia, kuna mtu katika mabwana wa huko alimtembelea ‘Umar. ‘Umar akamwulizia Uwais. Akamwambia: “Nimemwacha ana vyombo duni wala hana mali.” Akasema (Umar): “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Mutajiwa na Uwais bin ‘Âmir pamoja na makundi ya watu wa Yemen anaetoka katika kabila la Murâd kisha kutoka katika ukoo wa Qarni. Alikuwa ana mbalanga, akapona ela mahala kama dirhamu tu, ana mama anayemfanyia hisani kubwa. Lau atamwapia Allâh (ili Amfanyie jambo) basi Angalimfanyia. Ukiweza kumwambia akuombee maghfira, basi fanya hivyo.” Akamwendea Uwais, akamwambia: “Niombee maghfira.” Uwais akamwambia: “Wewe umekuja hivi karibuni kutoka safari njema (ya Hajj), niombee maghfgira. Umekutana na ‘Umar?” Akamjibu: “Ndio.” Akamwombea maghfira. Watu wakamfahamu (kuwa dua zake ni kabuli). Akatoka nje ya nchi.” [Imepokewa na Muslim.]
Riwaya nyingine ya Muslim pia imesema: “Usair bin Jâbir Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: “Watu wa al-Kûfah (‘Iraq) walimtembelea ‘Umar bin al-Khattâb Radhi za Allah ziwe juu yake , na miongoni mwao alikuwepo mtu aliyekuwa akimfanyia maskhara Uwais. ‘Umar akauliza: “Hapa kuna yeyote anaetokana na ukoo wa Qarni?” Mtu huyo akaja. ‘Umar akasema: “Mtume ﷺ amesema: “Hakika kuna mtu atakayewajia kutoka Yemen anayeitwa Uwais, hakuacha mtu huko Yemen ispokuwa mama yake. Alikuwa ana mbalanga, akamwomba Allâh, Akamwondolea (ugonjwa huo) ispokuwa sehemu ndogo kama dirhamu, atakayekutana naye miongoni mwenu, basi amwambie awaombee maghfira.”
Riwaya yake nyingine imesema: “‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Nilimsikia Mtume ﷺ akisema: “Hakika tabiina aliye bora ni mtu anayeitwa Uwais, ana mama. Alikuwa ana mbalanga, basi mwambieni awaombee maghfira.”