0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

360. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwatembelea watu wa kheri, kuketi nao,Kusuhubina nao, Kuwapenda na kuomba kutembelewa nao….

 باب زيارة أهل الخير ومجالستهم وصحبتهم ومحبتهم وطلب زيارتهم والدعاء منهم وزيارة المواضع الفاضلة


وعن أنس – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ أَبُو بكر لِعُمَرَ – رضي الله عنهما – بَعْدَ وَفَاةِ رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -: انْطَلِقْ بِنَا إِلَى أُمِّ أيْمَنَ – رضي الله عنها – نَزُورُهَا كَمَا كَانَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – يَزُورُهَا، فَلَمَّا انْتَهَيَا إِلَيْهَا، بَكَتْ، فَقَالاَ لَهَا: مَا يُبْكِيكِ؟ أمَا تَعْلَمِينَ أنَّ مَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لرَسُولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَتْ: مَا أبْكِي أَنْ لاَ أَكُونَ أَعْلَم أنَّ مَا عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرٌ لرسول الله – صلى الله عليه وسلم -، ولَكِنْ أبكي أنَّ الوَحْيَ قدِ انْقَطَعَ مِنَ السَّماءِ، فَهَيَّجَتْهُمَا عَلَى البُكَاءِ، فَجَعَلا يَبْكِيَانِ مَعَهَا.    رواه مسلم


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yao amehadithia: “Abûbakar alimwambia ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yao baada ya Mtume kuondoka duniani: “Tukamtembelee Ummu Ayman Radhi za Allah ziwe juu yake kama alivyokuwa Mtume akimtembelea.” Walipofika kwake, (Ummu Ayman) alilia. Wakamwuliza: “Jambo gani likulizalo, kwani hujui kuwa lililo kwa Allâh ndio kheri kwa Mtume ?” Akasema: “Mimi silii kwamba sijui kuwa lililo kwa Allâh ndio kheri kwa Mtume , lakini nalia kwa kuwa Wahyi umekatika (kuja kutoka) mbinguni.” Akawachochea kwa kilio, nao wakawa wanalia pamoja naye.” [Imepokewa na Muslim.]


Begin typing your search above and press return to search.