0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

344. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Fadhila Ya Kuwatendea Wema Marafiki Wa Baba Na Mama…

باب فضل بر أصدقاء الأب والأم والأقارب والزوجة وسائر من يندب إكرامه


وعن عائشة – رضي الله عنها -، قَالَتْ: مَا غِرْتُ عَلَى أحَدٍ مِنْ نِسَاءِ النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم – مَا غِرْتُ عَلَى خَدِيجَة – رضي الله عنها -، وَمَا رَأيْتُهَا قَطُّ، وَلَكِنْ كَانَ يُكْثِرُ ذِكْرَهَا، وَرُبَّمَا ذَبَحَ الشَّاةَ، ثُمَّ يقَطِّعُهَا أعْضَاء، ثُمَّ يَبْعثُهَا في صَدَائِقِ خَديجَةَ، فَرُبَّمَا قُلْتُ لَهُ: كَأنْ لَمْ يَكُنْ في الدُّنْيَا إلاَّ خَديجَةَ ‍! فَيَقُولُ: {إنَّهَا كَانَتْ وَكَانَتْ وَكَانَ لي مِنْهَا وَلَدٌ}   مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية: وإنْ كَانَ لَيَذْبَحُ الشَّاءَ، فَيُهْدِي في خَلاَئِلِهَا مِنْهَا مَا يَسَعُهُنَّ

وفي رواية:كَانَ إِذَا ذبح الشاة، يقولُ: {أَرْسِلُوا بِهَا إِلَى أصْدِقَاءِ خَديجَةَ}

وفي رواية: قَالَت: اسْتَأذَنتْ هَالَةُ بِنْتُ خُوَيْلِد أُخْتُ خَدِيجَةَ عَلَى رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، فَعرَفَ اسْتِئذَانَ خَديجَةَ، فَارتَاحَ لِذَلِكَ، فَقَالَ: {اللَّهُمَّ هَالةُ بِنْتُ خُوَيْلِدٍ}

قولُهَا: {فَارتَاحَ} هُوَ بالحاء، وفي الجمعِ بَيْنَ الصحيحين للحُميدِي: {فارتاع} بالعينِ ومعناه: اهتم بهِ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Âisha Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Sijawahi kumwonea wivu mke yeyote katika wakeze Mtume kama nilivyomwonea wivu (wivu ni ari ya kufanya jambo kama vile la kuondoa aibu na mfano wake) Bibi Khadija Radhi za Allah ziwe juu yake na ilihali sikumuona katu (maishani mwangu), lakini (Mtume) alikuwa akimtaja sana. Na mara nyingine alikuwa akichinja mbuzi, akimkata vipande vipande kisha akiwapelekea marifikize Khadija. Mara nyingine nilikuwa nikimwambia: “Kanakwamba duniani hakukuwa (na mwanamke) ela Khadija!” Basi hapo akisema: [ Alikuwa kadha wa kadha (akimsifu), na mimi nina watoto niliozaa naye.]    [Wameafikiana Bukhari na Muslim ].

Riwaya nyingine imesema: “(Mtume) alikuwa akichinja mbuzi na akiwapelekea marafikize (Khadija) kiasi kinachowatosha.”

Riwaya nyingine pia imesema: “Alikuwa anapochinja mbuzi husema: “Wapelekeeni marafikize Khadija.”

Riwaya nyingine, (‘Âisha) amesema: “Hâlah binti Khuwailid – dada yake Khadija – alibisha hodi kwa Mtume , (Mtume) akakumbuka hodi ya Khadija, akapendezewa na jambo hilo, akaomba: “Ewe Mola, Mjaalie awe ni Hâla binti Khuwailid.”


Begin typing your search above and press return to search.