باب بر الوالدين وصلة الأرحام
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص – رضي الله عنهما -، قَالَ: أقبلَ رَجُلٌ إِلَى نَبيِّ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: أُبَايِعُكَ عَلَى الهِجْرَةِ وَالجِهَادِ أَبْتَغي الأجْرَ مِنَ الله تَعَالَى. قَالَ: {فَهَلْ لَكَ مِنْ وَالِدَيْكَ أحَدٌ حَيٌّ؟} قَالَ: نَعَمْ، بَلْ كِلاهُمَا. قَالَ: {فَتَبْتَغي الأجْرَ مِنَ الله تَعَالَى؟} قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: {فارْجِعْ إِلَى وَالِدَيْكَ، فَأحْسِنْ صُحْبَتَهُمَا} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ، وهذا لَفْظُ مسلِم
وفي رواية لَهُمَا: جَاءَ رَجُلٌ فَاسْتَأذَنَهُ في الجِهَادِ، فقَالَ: {أحَيٌّ وَالِداكَ؟}قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: {فَفيهِمَا فَجَاهِدْ}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullâh bin ‘Amri bin al-‘Âs Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: “Mtu mmoja alimkabili Mtume ﷺ akamwambia: “Nitakubai juu ya Hijra na kupigana Jihadi katika Njia ya Allâh nikitafuta ujira kutoka kwa Allâh.” Akamwuliza: “Je, katika wazazi wako yuko aliye hai?” Akajibu: Ndio, wote wako hai. Akamwuliza: “Unatafuta ujira kutoka kwa Allâh?” Akajibu: Ndio. Akamwambia: “Rudi kwa wazazi wako na uwafanyie wema. “ [Wameafikiana Bukhari na Muslim]
Na katika Riwaya nyingine ya Bukhârî na Muslim imesema: Alikuja mtu akamwomba (Mtume ﷺ) idhini ya kwenda kupigana Jihadi. Akamwuliza: “Wazazi wako wako hai?” Akajibu: Ndio. Akamwambia: “Kwao wao, pigana Jihadi.” (Yaani: kaketi nao kwa uzuri na uvumilivu).