0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

320. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wazazi Na Kuunga Kizazi (Undugu) 09

باب بر الوالدين وصلة الأرحام


وعن أنسٍ – رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ أَبُو طَلْحَةَ أكْثَرَ الأنْصَارِ بالمَدينَةِ مَالاً مِنْ نَخل، وَكَانَ أحَبُّ أمْوَاله إِلَيْهِ بَيْرَحاء، وَكَانَتْ مسْتَقْبَلَةَ المَسْجِدِ، وَكَانَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم – يَدْخُلُهَا، وَيَشْرَبُ مِنْ مَاءٍ فِيهَا طَيِّب، فَلَمَّا نَزَلَتْ هذِهِ الآيةُ: ﴿لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ﴾ [ آل عمران: 92 ] قَامَ أَبُو طَلْحَةَ إِلَى رسولِ الله – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالَ: يَا رَسُول الله، إنَّ الله تبارك وتَعَالَى، يقول: ﴿لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ﴾ وَإنَّ أَحَبَّ مَالِي إِلَيَّ بَيْرَحَاءُ، وَإنَّهَا صَدَقَةٌ للهِ تَعَالَى، أرْجُو بِرَّهَا وَذُخْرَهَا عِنْدَ الله تَعَالَى، فَضَعْهَا يَا رَسُول الله، حَيْثُ أرَاكَ الله. فَقَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {بَخ ! ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ، ذلِكَ مَالٌ رَابحٌ ! وقَدْ سَمِعْتُ مَا قُلْتَ، وَإنِّي أرَى أنْ تَجْعَلَهَا في الأقْرَبينَ}، فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ: أفْعَلُ يَا رَسُول الله، فَقَسَّمَهَا أَبُو طَلْحَةَ في أقَارِبِهِ وبَنِي عَمِّهِ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وسبق بيان ألفاظِهِ في باب الإنْفَاقِ مِمَّا يحب


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: “Abû Talha alikuwa ana mali nyingi ya mitende Madina kuwaliko Ansari wengine. Mali iliyompendeza zaidi ni shamba lililoko Bairahâ, na lilikuwa liko mkabala wa Msikiti (wa Mtume). Mtume alikuwa akiingia humo na akinywa maji yake tamu. Ilipoteremka Aya hii: “Hamtaweza kufikia wema (hasa) mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda..” Abû Talha alimwendea Mtume , akamwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Allâh Amekuteremshia: Hamtaweza kufikia wema (hasa) mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda.. Kwa yakini mali inipendezayo mno ni (shamba la) Bairahâ, nimelitoa sadaka kwa ajili ya Allâh nikitaraji kheri yake na akiba yake kwa Allâh, kwa hivyo Yâ Rasûlallâh, liweke Atakapokuonyesha Allâh. Mtume akamwambia: [Hongera! Hiyo ni mali iliyopata faida, hiyo ni mali iliyopata faida! Nimesikia ulivyosema. Mimi naona uwape jamaa zako.] Abû Talha akasema: “Nitafanya hivyo Yâ Rasûlallâh.” Abû Talha akaligawa kwa jamaa zake na binamu zake.” ]  [Wameafikiana Bukhari na Muslim]


Begin typing your search above and press return to search.