July 19, 2022
0 Comments
BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -: أن النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: {اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى، وَابْدَأ بِمَنْ تَعُولُ، وَخَيْرُ الصَّدَقَةِ مَا كَانَ عَنْ ظَهْرِ غِنىً، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ يُعِفَّهُ اللهُ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ يُغْنِهِ اللهُ} رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: [Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Anza kwa unayemlisha. Sadaka bora ni inayotolewa baada ya kubakisha kitu. Anayejizuwia (kuomba), Allâh humtosheleza, na mwenye kukinai, Allâh humkinaisha. ] [Imepokelewa na Bukhari.]