KINGA YA MUISLAMU
Alikuwa Mtume ﷺ akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaasw, na Suratul-Falaq, na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele.
akifanya hivyo mara tatu. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Mtume ﷺ amesema : [Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Allaah ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii Shaytwaan mpaka asubuhi]
[…..اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُـوَ الـحَيُّ القَيّـومُ لا تَأْخُـذُهُ سِنَـةٌ وَلا نَـوْمٌ ]
[Imepokewa na Bukhari.]
Amesema Mtume ﷺ [Anayesoma aya mbili za mwisho wa Suratul-Baqarah usiku zinamtosheleza]
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ) ( لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى
الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَآ أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِين
[Imepokelewa na Bukhari na Muslim.]
Mtume ﷺ pia amesema: [Akiamka mmoja wenu kutoka usingizini kisha akarudi basi akikukute kitanda kwa shuka yake mara tatu na amtaje Mwenyezi Mungu kwani hajui kilicho kuja baada yake. Na Akilala aseme:]
[ بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي ، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فارْحَـمْها ، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين ]
[Kwa jina lako Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili yako nitaunyanyua, na ukiizuia (ukiichukua) roho yangu basi irehemu na ukiirudisha basi ihifadhi kwa kile unacho wahifadhi nacho waja wako wema.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
اللّهُـمَّ إِنَّـكَ خَلَـقْتَ نَفْسـي وَأَنْـتَ تَوَفّـاهـا لَكَ ممَـاتـها وَمَحْـياها ، إِنْ أَحْيَيْـتَها فاحْفَظْـها ، وَإِنْ أَمَتَّـها فَاغْفِـرْ لَـها . اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ العـافِـيَة
[Ee Mwenyezi Mungu hakika Wewe umeiumba nafsi yangu nawe utaiua, ni kwako uhai wa nafsi yangu na ufaji wake, ukiipa uhai basi ihifadhi, na ukiifisha (ukiiua) basi isamehe. Ee Allaah hakika mimi nakuomba afya njema.] [Imepokea na Muslim na Ahmad.]
Alikuwa Mtume ﷺ akitaka kulala anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake kisha anasema:
اللّهُـمَّ قِنـي عَذابَـكَ يَـوْمَ تَبْـعَثُ عِبـادَك ] ثلاث مرات]
[Ee Mwenyezi Mungu nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakayo wafufua waja wako.]
Mara tatu [Imepokewa na Abuu Daud.]
[ بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا ]
[Kwa jina lako Ee Mwenyezi Mungu ninakufa na ninakuwa hai.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Mtume ﷺ amesema: [Hivi niwafahamishe juu ya kitu ambacho ni bora zaidi kuliko mtumishi wakati munapolala; Msabihini Allaah mara thelathini na tatu, kisha msifuni Allaah mara thelathini na tatu, na kisha mtukuzeni mara thelathini na tatu kwani kufanya hivi ni bora kwenu kuliko mtumishi.]
[سُبْـحانَ الله ] ثلاثاً وثلاثين
[Ametakasika Mwenyezi Mungu] Mara thelathini na tatu.
[أَلْحَمْدُ لِلَّه] ثلاثاً وثلاثين
[Sifa njema zote ni za Mwenyezi mungu] Mara thelathini na tatu.
[اللَّه أكْبَرُ] ثلاثاً وثلاثين
[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa] Mara thelathini na tatu. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
اللهم ربَّ السموات السبع،ورب العرش العظيم،ربنا ورب كل شيء، فالق الحب والنوى، ومُنزل التوراة والإنجيل والفرقان، أعوذ بك من شر كل شيء أنت آخذٌ بناصيته،اللهم أنت الأول فليس قبلك شيء،وأنت الآخر فليس بعدك شيء، وأنت الظاهر فليس فوقك شيء، وأنت الباطن فليس دونك شيء، اقض عنا الدَّيْنَ واغننا من الفقر
[Ee Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu saba na Mola wa arshi tukufu, Mola wetu na Mola wa kila kitu Mwenye kuichanua tembe ya mbegu na kokwa na alieteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan, najikinga kwako kutokana na shari ya kila kitu. Wewe ndie mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe ndie wa Mwanzo hakuna kabla yako kitu, nawe ndie wa Mwisho, hakuna baada yako kitu, na wewe ndiye uliewazi, hakuna juu yako kitu chochote na Wewe ndiye uliyefichika hakuna kilichojificha chini yako. Tulipie madeni yetu na utuepushe na ufakiri.] [Imepokew na Muslim.]
[الـحَمْدُ للهِ الَّذي أَطْـعَمَنا وَسَقـانا، وَكَفـانا، وَآوانا، فَكَـمْ مِمَّـنْ لا كـافِيَ لَـهُ وَلا مُـؤْوي]
[Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametulisha na ametunywesha na akatutosheleza na akatuhifadhi, ni wangapi ambao hawana wa kuwatosheleza wala wa kuwahifadhi.] [Imepokewa na Muslim.]
اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيبِ وَالشّـهادةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه، أَشْهـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ نَفْسـي، وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى نَفْسـي سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم
[Ee Mwenyezi Mungu mjuzi wa yaliyojificha na yaliyo wazi, Muumba wa mbingu na ardhi, mola wa kila kitu na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, najilinda kwako na shari ya nafsi yangu na shari ya Shaytwaan na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu.] [Imepokewa na Abuu Daud]
Ukitaka kulala tawadha wudhuu kama wa Swalah kisha lalia ubavu wako wa kulia kisha sema:
اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت
[Ee Mwenyezi Mungu nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nime uelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulicho kiteremsha na Mtume wako uliyemtuma.]
Amesema Mtume ﷺ [kwa mwenye kusema haya kisha ukifa utakuwa umekufa katika Uislamu.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
SIKILIZA NYIRADI ZA KULALA