BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امرَأتَهُ إِلَى فرَاشِهِ فَلَمْ تَأتِهِ، فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا، لَعَنَتْهَا المَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وفي رواية لهما: {إِذَا بَاتَت المَرأةُ هَاجِرَةً فِرَاشَ زَوْجِهَا لَعَنَتْهَا المَلاَئِكَةُ حَتَّى تُصْبحَ}
وفي رواية قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -: {والَّذِي نَفْسِي بيَدِهِ مَا مِنْ رَجُلٍ يَدْعُو امْرَأتَهُ إِلَى فِرَاشهِ فَتَأبَى عَلَيهِ إلاَّ كَانَ الَّذِي في السَّمَاء سَاخطاً عَلَيْهَا حَتَّى يَرْضَى عَنها}
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Mtume ﷺ amesema: [Mwanamume atakapomwita mkewe kitandani (ili alale naye) wala asiende, akalala (mume huyo) akiwa amemkasirikia (mkewe), Malaika watamlaani (mke huyo) mpaka apambaukiwe] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]
Na katika Riwaya nyingine ya Bukhârî na Muslim zimesema: Mwanamke anapopitiwa na usiku ilihali amekigura kitanda cha mumewe, Malaika humlaani mpaka asubuhi.
Na Riwaya nyingine imesema: Mtume ﷺ amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake! Mwanamume yeyote anaemwita mkewe kitandani mwake naye (mke) akamkatalia, kwa hakika Alie mbinguni Humkasirikia mwanamke huyo mpaka (mumewe) amwelee radhi.”