0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

276. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kuwafanyia Wema Wanawake Hadithi 04

BUSTANI YA WATU WEMA


وعن عمرو بن الأحوصِ الجُشَمي – رضي الله عنه -: أنَّهُ سَمِعَ النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم – في حَجَّةِ الوَدَاعِ يَقُولُ بَعْدَ أنْ حَمِدَ الله تَعَالَى، وَأثْنَى عَلَيهِ وَذَكَّرَ وَوَعظَ، ثُمَّ قَالَ: {ألا وَاسْتَوصُوا بالنِّساءِ خَيْراً، فَإِنَّمَا هُنَّ عَوَانٍ عِنْدَكُمْ لَيْسَ تَمْلِكُونَ مِنْهُنَّ شَيْئاً غَيْرَ ذلِكَ إلاَّ أنْ يَأتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ، فَإنْ فَعَلْنَ فَاهْجُرُوهُنَّ في المَضَاجِع، وَاضْرِبُوهُنَّ ضَرباً غَيْرَ مُبَرِّحٍ، فإنْ أطَعْنَكُمْ فَلا تَبْغُوا عَلَيهنَّ سَبيلاً؛ ألاَ إنَّ لَكُمْ عَلَى نِسَائِكُمْ حَقّاً، وَلِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقّاً؛ فَحَقُّكُمْ عَلَيهِنَّ أنْ لا يُوطِئْنَ فُرُشَكُمْ مَنْ تَكْرَهُونَ، وَلا يَأْذَنَّ في بُيُوتِكُمْ لِمَنْ تَكْرَهُونَ؛ ألاَ وَحَقُّهُنَّ عَلَيْكُمْ أنْ تُحْسِنُوا إِلَيْهِنَّ في كِسْوَتِهنَّ وَطَعَامِهنَّ}    رواه الترمذي، وَقالَ: {حديث حسن صحيح}


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa ‘Amri bin al-Ahwas al-Jushamy Radhi za Allah ziwe juu yake alimsikia Mtume akisema katika Hajjatulwadâ’ – baada ya kumhimidi Allâh, kumsifu na kuwaedhea watu – kisha akasema: [Fahamuni! Wafanyieni kheri wanawake, hakika wao ni mateka wenu, hamna mnachomiliki kwao ispokuwa ni hicho tu (kustarehe na kumhifadhi mumewe katika nafsi yake na mali yake) ispokuwa watakapotenda ubaya wa wazi, watakapofanya hivyo wagureni katika malazi, na muwapige pigo lisilokuwa baya, wakiwatii msiwatafutie njia (ya kuwafanyia udhia). Fahamuni! Hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu, na wake zenu wana haki juu yenu. Haki yenu inayowapasa wao ni kutomruhusu mnayemchukia kuketi katika viti vyenu, wala wasiwaruhusu kuingia majumbani mwenu mnayemchukia. Fahamuni! Na haki zao zinazowapasa nyinyi ni kuwafanyia hisani katika mavazi na chakula chao.]               [ Imepokewa na Tirmidhy, na akasema: Hadîth hii ni Hasan Sahih.    

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.