BUSTANI YA WATU WEMA
وعن مصعب بن سعد بن أَبي وقَّاص – رضي الله عنهما -، قَالَ: رَأى سعد أنَّ لَهُ فَضْلاً عَلَى مَنْ دُونَهُ، فَقَالَ النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم -: {هَلْ تُنْصرُونَ وتُرْزَقُونَ إلاَّ بِضُعَفَائِكُمْ} رواه البخاري هكذا مُرسلاً، فإن مصعب بن سعد تابعيٌّ، ورواه الحافظ أَبُو بكر البرقاني في صحيحه متصلاً عن مصعب، عن أبيه – رضي الله عنه
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Mus‘ab bin Sa’d bin Abî Waqqâs Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Sa’di alikuwa akidhani kuwa yeye ana ubora kwa walio chini yake. Mtume ﷺ akasema: [Hamtanusuriwa wala kuruzukiwa ela kwa (sababu ya) madhaifu wenu.] [Imepokewa na Bukhari ikiwa na hadith Mursal, kwa sababu Mus’ab ni taabiy (siswahaba) hakumuona Mtume, na imepokelewa vile vile na Al- Haafidh Abubakar Al Barqaawiy katika sihihi yake ikiipokea kutoka kwa Sa’ad kutoka kwa Mtume radhi za Allah ziwafikie wote]