KINGA YA MUISLAMU
اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،ومن عذاب جهنم،ومن فتنة المحيا والممات ،ومن شر فتنة المسيح الدجال
البخاري 2/ 102 ومسلم 1/ 412 واللفظ لمسلم
[Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakutaka unihifadhi na adhabu za kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-dajjaal.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،وأعوذ بك من فتنة المسيح الدجال،وأعوذ بك من فتنة المحيا والممات، اللهم إني أعوذ بك من المأثم والمغرم
البخاري 1/ 202 ومسلم 1/ 412
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya Masihi-dajjaal, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na dhambi na deni.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
اللهم إني ظلمت نفسي ظلماً كثيراً ، ولا يغفر الذنوب إلا أنت ، فاغفر لي مغفرة من عندك وارحمني إنك أنت الغفور الرحيم
البخاري 8/168 ومسلم 4/ 2078
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, dhulma kubwa, na hasamehe madhambi ila Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka Kwako, na unirehemu, hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
[ اللهم اغفر لي ما قدمت وما أخرت وما أسررت وما أعلنت وما أسرفت وما أنت أعلم به مني أنت المقدم وأنت المؤخر لا إله إلا أنت] مسلم 1/ 534
[Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe niliyoyatanguliza, na niliyoyachelewesha, na niliyoyafanya kisiri, na niliyoyafanya kwa dhahiri na niliyoruka mipaka, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi, Wewe ndiye mwenye kutanguliza na Wewe ndiye mwenye kuchelewesha, hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.] [Imepokewa na Muslim]
[ اللهم أعني على ذكرك ، وشكرك وحسن عبادتك]
أبو داود 2/ 86والنسائي 3/ 53 وصححه الألباني في صحيح أبو داود 1/ 284
[Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukukumbuka, na kukushukuru, na uzuri wa kukuabudu] [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Nnasai na kusahihishwa na Al-Baaniy katika Sunan Abii Daudu]
[ اللهم إني أعوذ بك من البخل وأعوذ بك من الجبن ، وأعوذ بك من أن أرد إلى أرذل العمر ، وأعوذ بك من فتنة الدنيا وأعوذ بك من عذاب القبر ] البخاري 6/35
[Ewe Mwenyezi Mungu najilinda Kwako kutokana na ubakhili, na najilinda kwako kutokana na uwoga, na najilinda kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na najilinda kwako kutokana na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi] [Impokewa na Bukhari]
[ اللهم إني أسألك الجنة وأعوذ بك من النار ]
أبو داود وانظر صحيح ابن ماجه 2/ 328
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba pepo na najilinda kwako kutokana na moto.] [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah]
اللهم بعلمك الغيب وقدرتك على الخلق أحيني ما علمت الحياة خيراً لي وتوفني إذا علمت الوفاة خيراً لي ، اللهم إني أسألك خشيتك في الغيب والشهادة ، وأسألك كلمة الحق في الرضا والغضب ، وأسألك القصد في الغنى والفقر ، وأسألك نعيماً لا ينفد ، وأسألك قرة عين لا تنقطع ، وأسألك الرضا بعد القضاء ، وأسألك برد العيش بعد الموت ، وأسألك لذة النظر إلى وجهك والشوق إلى لقائك من غير ضرَّاء مضرة ولا فتنة مضلة ، اللهم زينا بزينة الإيمان ، واجعلنا هداة مهتدين
النسائي 4/54،55وأحمد 4/364 وصححه الألباني في صحيح النسائي 1/ 281
[Ewe Mwenyezi Mungu , kwa ujuzi Wako wa mambo yaliyo fichikana, na uwezo Wako wa kuumba, niweke hai iwapo uhai ni bora kwangu, na nifishe iwapo kufa ni bora kwangu, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba khofu yako kwa siri na dhahiri na ninakuomba neno la haki wakati nimefurahi na wakati nimekasirika, na ninakuomba matumizi ya wastani wakati wa utajiri na wakati wa umaskini, na ninakuomba neema isiyokwisha na ninakuomba kituliza jicho (moyo) kisicho katika, na ninakuomba kuridhia baada yakuwa umeshanipangia, na ninakuomba maisha ya utulivu baada ya kufa, na ninakuomba ladha ya kukutizama uso Wako, na shauku ya kukutana nawe, pasina madhara yanayodhuru, wala fitna yenye kupoteza. Ewe Mwenyezi Mungu tupambe kwa kipambo cha imani, na tujaalie tuwe waongozi wenye kuongoka.] [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ahmad na imesahihishwa na Al-Baaniy katika swahihi Al-Nnasaai]
[ اللهم إني أسألك يا الله بأنك الواحد الأحد الصمد الذي لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفواً أحد أن تغفر لي ذنوبي إنك أنت الغفور الرحيم ]
أخرجه النسائي بلفظه 3/52وأحمد 4/338 وصححه الألباني في صحيح النسائي 1/ 280
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba, Ewe Mwenyezi Mungu kwa vile Wewe ni Mmoja ulie pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote, nakuomba unisamehe makosa yangu hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe,, Mwenye kurehemu.] [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ahmad na imesahihishwa na Al-Baaniy katika swahihi Al-Nnasaai.]
اللهم إني أسألك بأن لك الحمد ، لا إله إلا أنت وحدك لا شريك لك ، المنان ، يا بديع السموات والأرض يا ذا الجلال والإكرام يا حي يا قيوم إني أسألك الجنة وأعوذ بك من النار
رواه أهل السنن وانظر صحيح ابن ماجه 2/ 329
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba, kwa vile sifa njema zote ni Zako, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali yakuwa pekeyako, huna mshirika, mwingi wa kuneemesha. Ewe Mtangulizi (muumbaji) wa mbingu na ardhi (bila kuwa na mfano kabla), Ewe mwenye Utukufu na ukarimu, Ewe Ulie hai mwenye kusimama kwa dhati Yako, hakika mimi nakuomba pepo , na najilinda kwako kutokana na moto.] [Imepokewa kwenye vitabu vya Sunna]
[اللهم إني أسألك بأني أشهد أنك أنت الله لا إله إلا أنت،الأحد الصمد الذي لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفواً أحد]
أبو داود2/62 والترمذي 5/ 515 وابن ماجه 2/ 1267 وأحمد 5/360 وانظر صحيح ابن ماجه 2/ 329 وصحيح الترمذي 3/ 163
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa vile ninakiri kwa hakika kwamba Wewe ni Mwenyezi Mungu hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa pekee, mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote] [Imepokewa na Abuu Daud, na Al-Ttirmidhiy, na Ibnu Maajah,na Ahmad ]