0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

245. Riyadhu Swalihina Mlango wa kuwakidhia Waislamu haja zao Hadithi 02


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن أَبي هريرة رضي اللَّه عنهُ ، عن النبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : « من نَفَّس عن مؤمن كُرْبة منْ كُرب الدُّنْيا ، نفَّس اللَّه عنْه كُرْبة منْ كُرَب يومِ الْقِيامَةِ ، ومنْ يسَّرَ على مُعْسرٍ يسَّرَ اللَّه عليْه في الدُّنْيَا والآخِرةِ ، ومنْ سَتَر مُسْلِماً سَترهُ اللَّه فِي الدنْيا والآخرة ، واللَّه فِي عوْنِ العبْد ما كانَ العبْدُ في عوْن أَخيهِ ، ومنْ سلك طَريقاً يلْتَمسُ فيهِ عِلْماً سهَّل اللَّه لهُ به طريقاً إلى الجنَّة . وما اجْتَمَعَ قوْمٌ فِي بيْتٍ منْ بُيُوتِ اللَّه تعالَى ، يتْلُون كِتَابَ اللَّه ، ويَتَدارسُونهُ بيْنَهُمْ إلاَّ نَزَلَتْ عليهم السَّكِينةُ ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمةُ ، وحفَّتْهُمُ الملائكَةُ ، وذكَرهُمُ اللَّه فيمَنْ عنده . ومنْ بَطَّأَ به عَملُهُ لمْ يُسرعْ به نَسَبُهُ »    رواه مسلم


Kutoka kwa Abuu Hurayra (Radhi za Allah ziwe juu yao) Amesema kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  Amesema: [Mwenye kumfariji dhiki Muislamu miongoni mwa dhiki za Duniani, Mwenyezi Mungu atamfariji dhiki miongoni mwa dhiki za siku ya Qiyama, Mwenye kumsahilishia mwenye uzito, Mwenyezi Mungu atamsahilishia duniani na Akhera, Mwenye kumsitiri Muislamu, Mwenyezi Mungu atamsitiri Duniani na Akhera, Mwenyezi Mungu yu katika kumsaidia mja maadamu mja huyo yu katika kumsaidia nduguye, Na mwenye kufuata njia akitafuta ilimu Mwenyezi Mungu atamsahilia njia ya kwenda Peponi. Wala watu hawatajumuika katika Nyumba miongoni mwa Nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakifundishana (kitabu hicho) ela huteremka utulivu kwao, wakifunikwa na Rehma, Malaika wakawazunguka na Mwenyezi Mungu Akawatja kwa walioko kwake. Na anaecheleweshwa kwa Amali yake hatopelekwa mbele kwa Nasaba yake] 
   [Imepokewa na Muslim]


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.