0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

211. MLANGO WA SUNNAH YA KUSUJUDU SIJDA YA KUSHUKURU WAKATI WA KUPATA NEEMA YA DHAHIRI AU KUONDOKEWA NA BALAA YA DHAHIRI


٢١١- باب استحباب سجُود الشكرعند حصول نعمة ظاهرة أَو اندفاع بلية ظاهرة


عَنْ سَعْدِ بنِ أَبي وَقَّاصٍ رَضِيَ اللَّه عنْهُ قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم مِن مَكَّةَ نُرِيدُ المَدِينَةَ، فَلَمَّا كُنَّا قَرِيبًا مِن عَزْوَراءَ نَزَلَ ثُمَّ رَفَعَ يَدَيْهِ، فدعَا اللَّه سَاعَةً، ثُمَّ خَرَّ سَاجِدًا، فَمَكَثَ طَوِيلاً، ثُمَّ قامَ فَرَفَعَ يَدَيْهِ، ساعَةً، ثُمَّ خَرَّ ساجِدًا فَعَلَهُ ثَلاثاً وَقَالَ: “إِنِّي سَأَلْتُ رَبِّي، وَشَفَعْتُ لأُمَّتِي، فَأَعْطَاني ثُلُثَ أُمَّتي، فَخَررتُ سَاجِداً لِرَبِّي شُكرًا، ثُمَّ رَفعْتُ رَأْسِي، فَسَأَلْتُ رَبِّي لأُمَّتي، فَأَعْطَانِي ثُلثَ أُمَّتي، فَخررْتُ سَاجِداً لربِّي شُكراً، ثمَّ رَفعْت رَأسِي فَسَألتُ رَبِّي لأُمَّتي، فَأعطاني الثُّلُثَ الآخَرَ، فَخَرَرتُ ساجِدا لِرَبِّي”     رواه أَبُو داود


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



211. MLANGO WA SUNNAH YA KUSUJUDU SIJDA YA KUSHUKURU WAKATI WA KUPATA NEEMA YA DHAHIRI AU KUONDOKEWA NA BALAA YA DHAHIRI


Imepokewa kutaka kwa Sa’d bin Abî Waqqâs ( Radhi za Allah ziwe juu yake)  amesimulia: “Tulitoka pamoja na Mtume Makkah tukielekea Madina. Tulipokuwa karibu na ‘Azwarâ, aliteremka kisha akainyanyua mikono yake, akamwomba Allâh kwa kitambo, kisha akapomoka kwa kusujudu, akatulia (katika sijda) mda mrefu, kisha akasimama, akainyanyua mikono yake kwa kitambo, kisha akapomoka kwa kusujudu. Alifanya hivyo mara tatu, na akaniambia: “Hakika nimemwomba Mola wangu na nimewaombea umati wangu (waingie Peponi), (Allâh) Akanipa thuluthi ya umati wangu, nikapomoka kwa kumsujudia Mola wangu kwa kushukuru, kisha nikainua kichwa changu, nikamwomba Mola wangu Awaingize Peponi umati wangu, Akanipa thuluthi ya umati wangu, nikapomoka kwa kumsujudia Mola wangu kwa kushukuru, kisha nikainua kichwa changu, nikamwomba Mola wangu Awaingize Peponi umati wangu, Akanipa thuluthi nyingine, nikapomoka kwa kumsujudia Mola wangu kwa kushukuru.”  [ Imepokewa na Abû Dâwûd. ]


Begin typing your search above and press return to search.