٢٠٩- باب استحباب ركعتين بَعْد الوضوء
عن أَبي هُريرةَ رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قالَ لِبلالٍ: “يَا بِلالُ حَدِّثْنِي بِأَرْجَى عَمَل عَمِلْتَهُ فِي الإِسْلامِ، فَإِنِّي سمِعْتُ دَفَّ نَعْلَيْكَ بيْنَ يَديَّ في الجَنَّة”قَالَ: مَا عَمِلْتُ عَمَلاً أَرْجَى عنْدِي مِنْ أَنِّي لَم أَتَطَهَّرْ طُهُوراً فِي سَاعَةٍ مِنْ لَيْلٍ أَوْ نَهارٍ إِلاَّ صَلَّيْتُ بِذلكَ الطُّهورِ مَا كُتِبَ لِي أَنْ أُصَلِّيَ“. متفقٌ عَلَيْهِ. وهذا لفظ البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
209. MLANGO WA SUNNAH YA KUSWALI RAKAA MBILI BAADA YA KUTAWADHA
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa Mtume ﷺ alimwambia Bilâl: “Ee Bilâl, nieleze amali uliyoitenda katika Uislamu unayoitarajia zaidi (malipo yake), kwani nilisikia sauti ya viatu vyako mbele yangu katika Pepo.” Bilâl akamwambia: “Sijatenda amali ninayoitarajia zaidi kama ambayo kila ninapotawadha wakati wowote ima iwe ni usiku au mchana, huwa nikiswali kwa udhu huo kiasi nilichojaaliwa kuswali.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim.]