١٩٧- باب تخفيف ركعتي الفجر وبيان مَا يقرأ فيهما، وبيان وقتهما
عنْ عائشةَ رَضِيَ اللَّه عَنْهَا أَنَّ النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، كانَ يُصَلي رَكْعتَيْنِ خَفِيفَتَيْنِ بَيْنَ النِّدَاءِ وَالإِقَامةِ مِن صَلاة الصُّبْحِ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وفي روايةٍ لهمَا: يُصَلِّي رَكعتَي الفَجْرِ، إِذَا سمِعَ الأَذَانَ فَيُخَفِّفُهمَا حَتَّى أَقُولَ: هَل قرَأَ فِيهما بِأُمِّ القُرْآنِ؟
وفي روايةٍ لمُسْلِمٍ: كَانَ يُصَلِّي ركعَتَي الفَجْرِ إِذَا سمِعَ الأَذَانَ ويُخَفِّفُهما
وفي روايةٍ: إِذا طَلَع الفَجْرُ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
197. MLANGO WA KUZIKHAFIFISHA RAKAA MBILI ZA ALFAJIRI, UBAINIFU WA KINACHOSOMWA NDANI YAKE NA UBAINIFU WA NYAKATI ZAKE
Imepokewa kutika kwa Âisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia kuwa: “Mtume ﷺ alikuwa akiswali rakaa mbili hafifu baina ya adhana na iqama katika Swala ya asubuhi.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].
Riwaya nyingine ya Bukhârî na Muslim imesema: “Akiswali rakaa mbili za alfajiri, anaposikia adhana huzikhafifisha mpaka nikijiuliza: kwani amesoma Alhamdu katika rakaa hizo!”
Riwaya nyingine ya Muslim imesema: “Alikuwa akiswali rakaa mbili za alfajiri akisikia adhana na akizikhafifisha.”
Riwaya nyingine imesema: “..inapotokeza alfajiri.”