١٩٤- باب فضلِ الصفِّ الأوَّلِ والأمرِ بإتمامِ الصفوفِ الأُولِ، وتسويِتها، والتراصِّ فِيهَا
عَن جابِرِ بْنِ سمُرةَ، رضي اللَّه عنْهُمَا، قَالَ: خَرجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَقَالَ: “أَلا تَصُفُّونَ كَمَا تُصُفُّ الملائِكَةُ عِنْدَ رَبِّهَا؟ “فَقُلْنَا: يَا رسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تَصُفُّ الملائِكةُ عِند ربِّها؟ قَالَ:“يُتِمُّونَ الصُّفوفَ الأُولَ، ويَتَراصُّونَ في الصفِّ” رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
194. MLANGO WA FADHILA ZA SAFU YA KWANZA, MAAMRISHO YA KUTIMIZA SAFU ZA KWANZA, KUZIWEKA SAWA NA KUKARIBIANA KATIKA SAFU
Imepokewa kutika kwa Jâbir bin Samurah ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesimulia: “Siku moja Mtume ﷺ alitutokea, akatwambia: “Hampangi safu kama vile Malaika wapangavyo safu kwa Mola wao?” Tukamwuliza: “Yâ Rasûlallâh, Malaika hupanga vipi safu kwa Mola wao?” Akajibu: “Wanatimiza safu za mwanzo na wanakribina katika safu (hawaachi mwanya).” [ Imepokewa Muuslim ].