0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

186. MLANGO WA FADHILA YA ADHANA (KUADHINI)


١٨٦- باب فضل الأذان


عَنْ أَبي هُريْرةَ رَضِيَ اللَّه عنْهُ أَنَّ رسُولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَال: “لَوْ يعْلمُ النَّاسُ مَا في النِّداءِ والصَّفِّ الأَولِ. ثُمَّ لَمْ يَجِدُوا إِلاَّ أَنْ يسْتَهِموا علَيهِ لاسْتهموا علَيْهِ، ولوْ يعْلَمُونَ مَا فِي التَّهْجِير لاسْتبَقوا إَليْهِ، ولَوْ يعْلَمُون مَا فِي العَتَمَةِ والصُّبْحِ لأتوهمُا ولَوْ حبواً”        متفقٌ عليه


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



186. MLANGO WA FADHILA YA ADHANA (KUADHINI)


Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira ( Radhi za Allah ziwe juu yake ) amesema: “Mtume amesema: “Lau watu wangalijuwa thawabu zipatikanazo katika kuadhini na safu ya kwanza, halafu wasipate njia ila kwa kupiga kura, basi wangalipiga kura juu yake. Na lau wanajua thawabu zipatikanazo katika kwenda mapema, basi wangalishindaniana, na lau wanajua thawabu ziliomo katika Swala ya Ishaa na Asubuhi, basi wangaliziendea hata kama ni kwa kusota.”    [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ]


Begin typing your search above and press return to search.