BUSTANI YA WATU WEMA
عن ابن عباس ، رضيَ اللَّه عنهما ، قال : قَامَ فينَا رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بمَوْعِظَةٍ فقال : « أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ محشورونَ إِلَى اللَّه تَعَالَى حُفَاةَ عُرَاةً غُرْلاً { كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُعِيدُهُ وَعْداً علَيْنَا إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ } [ الأنبياء : 103] أَلا وَإِنَّ أَوَّلَ الْخَلائِقِ يُكْسى يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِبراهيم صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، أَلا وإِنَّهُ سَيُجَاء بِرِجَالٍ مِنْ أُمَّتِى، فَيُؤْخَذُ بِهِمْ ذَاتَ الشِّمال فأَقُولُ: يارَبِّ أَصْحَابِي ، فيُقَالُ : إِنَّكَ لا تَدْرِي مَا أَحْدَثُوا بَعْدَكَ ، فَأَقُول كَما قَالَ الْعَبْدُ الصَّالِحُ : { وكُنْتُ عَلَيْهمْ شَهيداً ما دُمْتُ فِيهمْ } إِلَى قولِهِ : { العَزِيز الحَكيمُ } [ المائدة : 117 ، 118 ] فَيُقَالُ لِي : إِنَّهُمْ لَمْ يَزَالُوا مرْتَدِّينَ عَلَى أَعقَابِهِمْ مُنذُ فارَقْتَهُمْ » متفقٌ عليه
Kutoka kwa Ibin ‘Abbaas Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtumealisimama na kututolea mawaidha akasema: [Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Mwenyezi Mungu haliyakuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa (na magovi). [Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu, bila shaka Sisi ni wenye kufanya (Tusemayo).] [Al-Anbiyaa: 104]
Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabii Ibrahim (‘Alayhis salaam). Tanabahini! Wataletwa watu katika Umma wangu na watapelekwa upande wa kushoto (motoni), Nami nitasema: “Ewe Mola wangu, Maswahaba wangu!” Nitaambiwa: “Wewe hujui watu hawa walichokizua baada yako. [Hapo nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabii ‘Issa) [Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao.] Akasoma mpaka: “Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” [Al-Maaida: 117-118]. Nitaambiwa: “Wao waliendelea kugeuka nyuma kwa visigino vyao tangu ulipowaacha.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]