0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

165. MLANGO WA KULIA NA KUWA NA KHOFU WAKATI WA KUPITA KATIKA MAKABURI YA MADHALIMU NA SEHEMU ZAO WALIZOANGAMIZWA, KUDHIHIRISHA UHITAJI KWA ALLÂH NA MAONYO YA KUGHAFILIKA NA JAMBO HILO

باب البكاء والخوف عند المرور بقبور الظالمين ومصارعهم وإظهار الافتقار إِلَى الله تَعَالَى والتحذير من الغفلة عن ذلك


عَن ابْنِ عُمَر رَضِيَ اللَّه عَنْهُمَا أَنَّ رسُولَ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قَالَ لأصْحَابِهِ يَعْني لمَّا وَصلُوا الحِجْرَ: دِيَارَ ثمُودَ: “لاَ تَدْخُلُوا عَلى هَؤُلاءِ المُعَذَّبِينَ إِلاَّ أَنْ تَكُونُوا بَاكِينَ، فَإِنْ لمْ تَكُونُوا باكِين، فَلا تَدْخُلُوا عَلَيْهِمْ، لاَ يُصِيبُكُمْ مَا أَصَابَهُمْ”        متفقٌ عليه

وفي روايةٍ قَالَ: لمَّا مَرَّ رَسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بِالحِجْرِ قَالَ: “لاَ تَدْخُلُوا مَسَاكِنَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ أَنْ يُصِيبكُمْ مَا أَصَابَهُمْ إِلاَّ أَنْ تَكُونُوا بَاكِينَ” ثُمَّ قَنَّع رَسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، رَأْسَهُ وَأَسْرَعَ السَّيْرَ حَتى أَجَازَ الوَادي


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



165. MLANGO WA KULIA NA KUWA NA KHOFU WAKATI WA KUPITA KATIKA MAKABURI YA MADHALIMU NA SEHEMU ZAO WALIZOANGAMIZWA, KUDHIHIRISHA UHITAJI KWA ALLÂH NA MAONYO YA KUGHAFILIKA NA JAMBO HILO


Imepokewa na ‘Abdullâh bin ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yao)  amesimulia kuwa Mtume aliwaambia Maswahaba zake – walipofika al-Hijri – katika majumba ya Thamûd: “Msiingie kwa hawa walioadhibiwa ela muwe mnalia, msipokuwa ni wenye kulia musiingie musije mukapatwa na lililowapata wao.”     [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].

Riwaya nyingine imesema: “Mtume alipopita al-Hijri, alisema: “Musiingie katika maskani ya wale waliodhulumu nafsi zao musije mukapatwa na lililowapata wao ela muwe ni wenye kulia.” Kisha Mtume akajifunika kichwa chake kwa kitambaa, na akaharakisha mwendo mpaka akalivuka jangwa.”


Begin typing your search above and press return to search.