December 4, 2024
0 Comments
باب فضل من مات لَهُ أولاد صغار
عن أنس رضي اللَّه عَنْه قَالَ: قَال رَسولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “مَا مِنْ مُسلِمٍ يَمُوتُ لَهُ ثلاثَةٌ لَمْ يَبلُغُوا الحِنْثَ إِلاَّ أدخلَهُ اللَّه الجنَّةَ بِفَضْل رحْمَتِهِ إيَّاهُمْ”. متفقُ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
164. MLANGO WA FADHILA ZA ALIYEFIWA NA WATOTO WADOGO
Imepokewa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Muislamu yeyote atakayefiwa na watoto watatu ambao hawajafikia umri wa kubaleghe, Allâh Atamwingiza Peponi kwa fadhila ya rehema Yake kuwarehemu wao.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].