باب ثناء الناس عَلَى الميت
عن أَنسٍ رضي اللَّه عنه قَالَ: مرُّوا بجَنَازَةٍ، فَأَثنَوا عَلَيْهَا خَيراً فَقَالَ النبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:“وَجَبَتْ”، ثُمَّ مرُّوا بِأُخْرَى، فَأَثنَوْا عَلَيْهَا شَرّاً، فَقَال النَِّبيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم:“وَجبَتْ”فَقَال عُمرُ بنُ الخَطَّاب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ: ما وجبَتْ؟ قَالَ:“هَذَا أَثنَيتُمْ علَيْهِ خَيراً، فَوَجبتْ لَهُ الجنَّةُ، وهَذَا أَثنَيتُم عَلَيْهِ شَرّاً، فَوَجبتْ لَهُ النًَّارُ، أنتُم شُهَداءُ اللَّهِ في الأرضِ”. متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
163. MLANGO WA WATU KUMSIFU MAITI
Imepokewa na Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Watu walipita na jeneza, Maswahaba wakalisifu kwa wema, Mtume ﷺ akasema: “Limepasa.” Kisha wakapita na jeneza lingine, wakalisifu kwa ubaya, Mtume ﷺ akasema: “Limepasa.” ‘Umar bin al-Khattâb (Radhi za Allah ziwe juu yake) akauliza: “Ni kitu gani kilichopasa?” Mtume ﷺ akasema: “Huyu mumemsifu kwa wema akapasa kuingia Peponi, na yule mumemsifu kwa ubaya akapasa kuingia motoni. Nyinyi ndio mashahidi wa Allâh ulimwenguni.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].