0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

162. Riyadhu Swalihina Mlango wa kuzihifadhi Sunna na Adabu zake Hadithi ya 07


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين 


عن أَبِي موسى رضي اللَّه عنه قال : قال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « إِنَّ مَثَل مَا بعَثني اللَّه بِهِ منَ الْهُدَى والْعلْمِ كَمَثَلَ غَيْثٍ أَصَاب أَرْضاً فكَانَتْ طَائِفَةٌ طَيبَةٌ ، قبِلَتِ الْمَاءَ فأَنْبَتتِ الْكلأَ والْعُشْبَ الْكَثِيرَ ، وَكَانَ مِنْهَا أَجَادِبُ أَمسكَتِ الماءَ ، فَنَفَعَ اللَّه بها النَّاس فَشَربُوا مِنْهَا وسَقَوْا وَزَرَعَوا. وأَصَابَ طَائِفَةً أُخْرَى ، إِنَّمَا هِيَ قِيعانٌ لا تُمْسِكُ ماءً وَلا تُنْبِتُ كَلأ فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقُهَ فِي دِينَ اللَّه ، وَنَفَعَه ما بعَثَنِي اللَّه به ، فَعَلِمَ وعَلَّمَ، وَمثلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذلِكَ رَأْساً وِلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللَّهِ الذي أُرْسِلْتُ بِهِ »    متفقٌ عليه


Kutoka kwa Abuu Musaa Radhi za Allah ziwe juu yake Amesema: Amesema: Mtume[Mfano wa Aliyonituma kwayo Mwenyezi Mungu katika uongofu na elimu, ni mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika nchi, ikawa ina rutuba, ikakubali maji, ikaotesha nyasi na maji mengi. Na sehemu nyingine ikawa ni kavu na ngumu inayozuia maji, Mwenyezi mungu Akawanufaisha watu kwa mvua hiyo. Wakanywa, wakanywesha mifugo na kulimia kwayo. Na ikanyesha sehemu nyingine ambayo ni kavu haizuii maji, wala haioteshi nyasi. Basi mifano hiyo ni mfano wa mtu aliyekuwa na ufahamu mzuri katika Dini ya Mwenyezi Mungu, yakamnufaisha yale Aliyonituma kwayo Allaah, akajifunza na akafundisha. Na mfano wa mwisho ni mfano wa mtu ambaye, hakuinua kichwa kwa jambo hilo na wala hakuukubali uongofu wa Mwenyezi Mungu niliyotumwa nao.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.